KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

October 2, 2014

FAINALI DANCE% KUTIMUA VUMBI JUMAMOSI

Displaying 001.Dance.jpg
Meneja wa Uhusiano wa Umma  wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kulia), akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam jana juu ya fainali  ya mashindano hayo yatakayofanyika jumamosi Don Bosco Oysterbay jijini. Kulia ni Mratibu wa shindano  hilo la Dance 100%, Happy Shame.
Displaying DANCE_02.JPG 
Mratibu wa shindano la Dance 100%, Happy Shame ( kushoto), akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam jana. Juu ya fainali  ya shindano hilo  litakalofanyika jumamosi Don Bosco Oysterbay  Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Meneja Uhusioano wa Umma  wa Vodacom Tanzania Matina Nkurlu.

Fainali za Dance100%  kutimua vumbi Jumamosi

Na Mwandishi Wetu

FAINALI za shindano la kucheza muziki maarufu kama Dance 100% linalofanyika chini ya uratibu wa Kituo cha East Africa Television ltd  na kudhaminiwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania, zitanayika Jumamosi hii ya Oktoba 4, Viwanja vya Don Bosco, Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa shindano hilo Happy Shame alisema jijini Dr es Salaam jana kuwa, fainali za shindano hilo ambalo safari yake ilianza Julai 19, mwaka huu kuanzia hatua ya kusaka washiriki hadi mchujo litashirikisha makundi matano.

Alisema kutokana na kila kundi kutaka kuibuka mshindi na kujitwalia kitita cha sh mil 5, kwa muda mrefu yamekuwa yakijifua kuhakikisha wanafanya kweli siku hiyo mbele ya jopo la majaji wakiongozwa na Super Nyamwela.

Shame alisema, shindano la mwaka huu limekuwa na msisimko wa aina yake zaidi kuliko miaka miwili iliyopita baada ya mambo mbalimbali kuboreshwa na zaidi kiasi cha vijana kuona ni fursa kwao sio tu kupata fedha, pia kuendeleza vipaji vyao.

“Ushindani umekuwa mkubwa sana katika shindano la mwaka huu ikilinganishwa na miaka mingine kutokana na sababu mbalimbali.  Shindano pia limeanza kupata mashabiki, tunashukuru sana sapoti ya wadhamini wetu Vodacom Tanzania,” alisema.
 
Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu,alieleza kuwa  mbali ya dau hilo kwa mshindi, kila mshiriki pia atapatiwa simu iliyounganishwa na  mtandao wa Vodacom.

Nkurlu alisema jana kuwa, kundi litakaloibuka nafasi ya pili katika fainali hiyo, litajipatia zawadi ya sh Milion 1.5 na mshindi wa tatu atapata kiasi cha laki 5.

Alisema kampuni ya Vodacom inajivunia kudhamini shindano hilo kwa njia hiyo ya udhamini wakitambua umuhimu wa vijana kujiajiri kupitia vipaji vyao na kuongeza kuwa, kwa kipindi chote cha mchakato wa shindano hilo, vijana wamejifunza mengi.

“Vijana wameonyesha uwezo mkubwa kuanzia hatua ya mchujo hadi sasa kiasi cha kuwapa majaji wakati mgumu. Tunaamini hata baada ya fainali, vijana hawa watajiendeleza zaidi kimuziki,” alisema Nkurlu.

Makundi hayo matano yaliyoingia hatua ya fainali, vijana wamekuwa wakionesha vipaji na umahiri mkubwa wa kucheza staili mbalimbali za muziki ambayo ni Wazawa Crew, Best Boys Crew, The W.T, Wakali Sisi na The winners Crew.

Nkurlu aliongeza kuwa, kwa vile vijana hao wamejiweka katika mazingira ya kutumia vipaji vyao kujipatia ajira, Kampuni ya Vodacom-Tanzania inaona fahari kudhamini shindano hilo wakisaidia juhudi za serikali kupambana na tatizo la ajira.

“Takwimu zinaonesha kuwa kila mwaka vijana zaidi ya 800,000 wanaingia katika soko la kusaka ajira ndio maana, Vodacom Tanzania kwa kulitambua hilo, tumekuwa mstari wa mbele kusaidiana na serikali na wadau wengine kuwajengea vijana msingi,” alisema Nkurlu.

Kuhusu zawadi, Nkurlu alisema kundi litakaloibuka mshindi, litaondoka nash mil 5, huku kila mshiriki katika katika kundi hilo akipatiwa simu aina ya Vodafone ikiwa na muda wa maongezi wa sh. 100,000.

MWISHO.


Finals for Dance100% now scheduled for October 4th

By Staff reporter 

THE finals for Dance 100% competition is now scheduled for 4th of October at Don Bosco grounds located in Oyster bay Dar es Salaam.

Sponsored by Vodacom Tanzania and coordinated by East Africa Television ltd, the finals will see five groups competing for top position.

The competition coordinator Happy Shame, said the tournament started in 19th July this year by searching for participants followed by quarter and semi finals.

She said, the five groups to compete in the finals have been working hard in their routine exercises as they are all eager to walk away with cash price amounting to Tsh 5 million.

Happy noted that, the judging desk was well prepared under the leadership of Super Nyamwela who is chief judge for the particular day.

The tournament coordinator further noted that, this year’s tournament have attracted a lot of youth to participate different from the past two years due to improvement made adding that the participants have come to realize that apart from making money the competition are ideal platform to  develop their talents. 

"The groups have been competing very hard in this year’s competition different from the past years due to number of reasons. Turnout for fans have also been very impressive, a lot of thanks should go to our sponsor Vodacom” she added

On his part, Vodacom Tanzania Public Relations Manager Matina Nkurlu said apart from the grand prize, every participant will be awarded a mobile phone exclusive connected to Vodacom network loaded with airtime worth 100,000/-.

Nkurlu admitted that, the second winner in the competition will walk away with cash prize amounting to Tsh 1.5 million and the third winner will get Tsh 500,000/-

He said, Vodacom was proud to sponsor the tournament because it believes in empowering youths in various ways including enabling to employ themselves through their talents adding that, through the competition the participants have learn a lot of issues.

“The youths have shown extra ordinary skills from day one of this competition. As a result, the judges have been in hard time. It’s our sincere hope that, from here the participants will keep on developing their talents, he said.

The five groups to compete in the finals include Wazawa Crew, Best Boys Crew, The W.T, Wakali Sisi and The winners Crew.

“Statistics shows that, every year over 800,000 youths gets into labor market but the market is not able to absolve them all. This is why Vodacom have decided to sponsor the tournaments as effort to complement the government and other stakeholders to enable the youths employ themselves through their talents,” Added Nkurlu 

ENDS.

No comments:

Post a Comment