KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

October 20, 2014

HOTEL ZA DOUBLE TREE BY HILTON TANZANIA WADHAMINI SIKU YA CHAKULA


Hotel Za Double Tree By Hilton Tanzania, Tarehe 18.10.2014 walidhamini Siku Ya Maonesho Ya chakula, yalliyofanyika kwenye viwanja vya shule ya Tanganyika International Schools. Pichani Juu Katikati ni Meneja Masoko wa Hotel za Double Tree By Hilton, Bw. Florenso Kirambata, kushoto ni mpishi mkuu wa Double Tree, Hassan na kulia ni Ayman.

Akielezea madhumuni ya kuandaa siku hiyo  Mkurugenzi wa Mauzo  wa Hotel za Double Tree By Hilton Tanzania, Bw. Florenso Kirambata; alisema kuwa nia yao kubwa ni kuweza kuzipatia fursa makampuni mbali mbali na wajasiliamali wadogo wadogo kuweza kuonyesha uwezo wao na bidhaa wanazotengeneza.
 
Mr Florenso  akaongeza kuwa zaidi ya wajasiriamali wadogo wadogo 100(mia Moja) na Wakubwa 50(hamsini) walishiriki kwenye maonesho hayo hasa lengo kuu ikiwa ni kuonesha aina mbali mbali za vyakula wanavyozalisha hivyo kuweza kujitangaza na kufahamika


Mpishi Msaidizi wa Hotel ya Double Tree,  Awadh (kushoto), akiwa Anapata maelekezo toka kwa Mpishi mwenzake, Ayman, namna ya kuandaa na kuchanganya vyakula
Mpishi Mkuu wa Hotel za Double tree, Bw. Hassan, akitoa maelekezo kwa wasaidizi wake 
Meneja Masoko wa Hotel za Double Tree By Hilton, Bw. Florenso Kirambata, akiwa na wapishi wa Hotel za Double Tree, wakipata maelekezo kwa mmoja wa washiriki wa maonesho ya chakula
Wapish wa Hotel Za Double Tree Wakiangali moja ya Bidhaa Toka kwa mshiriki wa maonesho ya siku ya chakula
Mwaandaaji mku wa Maonesho hayo wa kwanza Kulia akiwapa maelekezo wapishi wa Hotel za Double Tree 
Mpishi msaidizi wa Hotel za Double Tree, akiwapa maelekezo wateja waliotembelea banda lao namna chakula cha Hot Dog kinavyotengenezwa
 Banda la American Garden, walikuwepo nao kuonyesha bidhaa zao tofauti tofauti

No comments:

Post a Comment