KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

October 20, 2014

REDIO 5 WAWAKUTANISHA WANASALAMU KUTOKA MIKOA ZAIDI YA 21

SAM_0706
Baadhi ya Wanasalamu wa kituo cha Redio 5 chenye makao yake makuu njiro jijini Arusha, wakikabidhi sehemu ya msaada wao kwa uongozi wa hospitali ya mkoa Mt. Meru jana, kulia ni Mratibu wa salamu kupitia kipindi cha usiku wa moto, Yacob Simba, kushoto ni Sista Shubi Mjawizi, anayefatia ni Sista Merry Stalla
SAM_0705
Yacob Simba, akiongea na baadhi ya wanasalamu katika viwanja vya hospitali ya Mt. Meru, anayefatia ni Godfrey Thomas, ambao ni Mratibu wa shughuli hiyo kupitia kituo cha Redio 5 katika kipindi cha usiku wa moto, kinachorushwa kuanzia saa saba usiku hadi kumi na moja alfajiri kwa wiki nzima
SAM_0710
Yacob Simba, akikabidhi ndoo ya mafuta  kwa uongozi wa hospitali ya Mt. Meru, jana baadaa ya wanasalamu kutoka mikoa zaidi 21 kufika hospitalini hapo kuwafariji wagonjwa
SAM_0696
Vicky Mwakoyo, ambaye ni Creative Meneja wa kampuni ya  Tan Communication Media, inayomiliki kituo cha Radio 5 Arusha, katikati ni Yacob Simba na Godfrey Thomas wakiwa wakijadili jambo
SAM_0692
Sehemu ya msaada uliotolewa na wanasalamu kwa wagonjwa hospitali ya Mt.Meru jijini Arusha
SAM_0703
Kushoto Mtangazaji maarufu wa Redio 5 kupitia kipindi chake cha  love cuts, kinachorushwa jumatatu hadi ijumaa saa nne  hadi saa saba usiku, Semio Sonyo,  akiwa na mtangazaji machachari aliyejizolea umaarufu mkubwa kupitia kipindi chake cha usiku wa Moto, kinachorushwa kuanzia saa saba usiku hadi kumi na moja alfajiri kwa wiki nzima, Godfrey Thomas aka GT, wakifurahia jambo
SAM_0715
Nesi wa hospitali ya Mt.Meru, Sista Merry Stella, akitoa neno la shukrani kwa wanasalamu waliofika kuwatembela wagonjwa hospitalini hapo, ambapo amewataka watu na mashirika mbalimbali kuiga mfano huo kwa kuwa mahitaji ya wagonjwa ni makubwa
SAM_0721
Muonekano katika hospitali ya Mt.Meru jijini Arusha
SAM_0794
Wanasalamu wakiwa wamevalia T-sheti za Redio 5
SAM_0776
Wapili kulia ni mmiliki wa jamiiblog, Pamela Mollel, wakwanza kushoto ni Godfrey Thomas aka GT, wakiwa katika picha na baadhi ya wanasalamu jana, zoezi hilo liliratibiwa na kituo cha Redio 5 kupitia kipindi cha usiku wa moto
SAM_0728
Baadhi ya wanasalamu wakisubiria kuingia katika wodi mbalimbali kuwajulia hali wagonjwa hospitalini hapo
SAM_0730
“Pole mama Mungu atakuponya”hayo ni maneno ya wanasalamu"
SAM_0734
Yacob Simba, mtangazaji wa Redio 5, akiwa anamjulia hali mama mgonjwa katika wodi ya wanawake
SAM_0741
Mwanasalamu mkongwe kutoka Arusha, Baba Ali Mbondei (aliyevalia tisheti ya Redio 5), akiwa na wanasalamu wenzake wakimjulia hali mgonjwa katika wodi ya wanaume
SAM_0742
Wanasalamu wakiwa wanasoma dua kwa mgonjwa wodi ya wanaume katika hospitali ya Mt.Meru jijini Arusha
SAM_0746
Wanasalamu wakiwa wanaingia wodi ya saba kuwaona wagonjwa
SAM_0752
Godfrey Thomas  aka GT katikati akiwa amepozi na mashabiki wake ambao ni wanasalamu kupitia kipindi cha usiku wa moto cha kituo cha Redio 5 jijini Arusha
SAM_0749 
Wanasalamu kutoka mikoa mbalimbali wakiwa katika picha ya pamoja katika viwanja vya hospitali ya Mt.Meru, mara baada ya kufanya ziara ya kuwatembelea wagonjwa

No comments:

Post a Comment