KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

October 28, 2014

JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI YANDAA MAFUNZO YA SIKU TANO KWA BODI YA CHAKULA, DAWA NA VIPODOZI ZANZIBAR

unnamed
Mratibu wa Mafunzo ya kuwajengea Uwezo Watendaji wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi, Patrick Mwesigye, kutoka nchini Rwanda, akitoa nasaha zake kwa Watendaji hao katika uzinduzi wa mafunzo hayo katika Ukumbi wa Hoteli ya Ocean View.
  unnamed3 
Mgeni rasmi Msajili wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar, Dkt. Burhan Othaman Simai (katikati), waliokaa akiwa katika Picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya siku tano ya kuwajengea uwezo watendaji wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi, ambayo yanalenga kuanzisha Chombo maalum cha pamoja cha Usajili wa Dawa katika nchi Wanachama wa Afrika Mashariki.


Na Mwandishi wetu.

Jumuiya ya Afrika Mashariki imeandaa Mafunzo ya kuwajengea uwezo Watendaji wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar  ikiwa ni Mkakati wa kuunda Chombo maalum cha pamoja cha usimamizi na usajili wa Dawa utakaofanywa katika nchi Wanachama wa Jumuiya hiyo.

Mafunzo hayo ya siku tano yanalengo la kuweka Msimamo wa Pamoja na Viwango sawa kwa Bodi za Vyakula na Dawa ili Dawa itakaposajiliwa katika nchi moja ikubalike kimatumizi katika nchi wanachama wa Afrika Mashariki.

Akizungumza katika uzinduzi wa mafunzo hayo katika ukumbi wa Hoteli ya Ocean View Msajili wa Bodi ya Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar, Dkt. Burhan Othaman Simai, amesema kuwepo kwa chombo cha usimamizi wa pamoja katika nchi hizo kutasaidia kuondokana  na tatizo la uingizwaji wa Dawa zisizofaa Kimatumizi katika nchi hizo.

Amesema, hombo hicho kitasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza tatizo hilo kwa vile kutakuwa na mikakati ya kupeana taarifa za karibu kuhusu Dawa zinazosajiliwa na kusambazwa katika nchi zao.

Kwa upande wake Mratibu wa Mafunzo hayo, Patrick Mwesigye, kutoka nchini Rwanda, amesema malengo ya jumuiya hiyo ni kuhakikisha vitengo vyote vya nchi wanachama vinajengewa uwezo na ufanisi ili viwe katika ubora unaofanana.

Amesema kwa sasa kila nchi inatathmini na kusajili Dawa kivyake na kwamba kukamilika kwa mafunzo hayo itakuwa ni hatua kubwa ya kufikia makubalianao ya kuanzishwa kwa chombo kimoja cha usajili wa Dawa katika nchi wanachama wa Afrika Mashariki.

Akizungumza pembeni ya Mkutano huo Mratibu mwenza kutoa Zanzibar,  Hidaya Juma Hamad, amesema kukamilika kwa chombo hicho kutasaidia sana upatikanaji wa Dawa salama katika nchi husika.

Amesema sambamba na hilo kutasaidia kupunguza gharama na matumizi mengi ya rasilimali ambayo yangetumika katika nchi zingine.

“Dawa moja kuisajili inaweza kuchukua miaka miwili kwa hiyo Dawa hiyo itakaposajiliwa katika nchi moja itakuwa na uhalali wa kutumika katika nchi nyingine bila kusajiliwa tena, na hapo gharama kubwa zitakuwa zimeepukwa” Alisema Hidaya.

Pamoja na Zanzibar kupewa mafunzo hayo bado inakabiliwa na Changamoto nyingi zinazokwaza ufanisi wao ikiwemo uhaba wa Fedha, Ofisi ndogo na idadi ndogo ya wataalamu na watendaji wa kukagua maduka ya Dawa, Vyakula na upekuzi bandarini.

No comments:

Post a Comment