Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea,
Mathias Chikawe (kushoto), akimkabidhi Kapteni wa Timu ya Mpira wa Miguu
ya Ubungo Stars ya Kata ya Namapwia, Wilayani Nachingwea, Hassan Abbas,
zawadi ya mpira wa miguu baada ya timu hiyo kuongoza ligi katika Kata
hiyo. Timu nne zilishiriki mashindano hayo ya Kata na kufanikiwa
kutengeneza timu moja ambayo itashiriki katika mashindano ya Tarafa ya
Ruponda na baadaye kufika ngazi ya wilaya ambapo mshindi wa Wilaya
anatarajiwa kupewa zawadi nono ya Sh 500,000, itakayotolewa na Mbunge wa Jimbo hilo. Hata hivyo, Chikawe alitoa jezi seti 170, pamoja na mipira
100 kwa ajili ya timu 170 za mpira wa miguu zilizopo katika Jimbo hilo.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea,
Mathias Chikawe (kushoto) akimkabidhi Diwani wa Kata ya Namapwia,
wilayani Nachingwea, Sefu Mwenyewe fedha kwa ajili ya mshindi wa pili
pamoja na wasimamizi wa ligi hiyo. Katika mashindano hayo ya ligi
yaliyomalizika hivi karibuni, Timu ya Ubungo Stars iliibuka kidedea
katika kata hiyo na kufanikiwa kupewa zawadi ya mpira wa miguu. Timu nne
zilishiriki mashindano hayo kufanikiwa kutengeneza timu moja ambayo
itashiriki katika mashindano ya Tarafa ya Ruponda na baadaye kufika
ngazi ya wilaya ambapo mshindi wa wilaya anatarajiwa kupewa zawadi nono
ya Sh 500,000 itakayotolewa na Mbunge wa jimbo hilo. Hata hivyo, Chikawe
alitoa jezi seti 170 pamoja na mipira 100 kwa ajili ya timu 170 za
mpira wa miguu zilizopo katika jimbo hilo. Picha na Felix Mwagara.
Kapteni
wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Timu ya Ubungo Stars, Kata ya Nawapwia,
Hassan Abbas akimshukuru Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni
Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe (kushoto) kwa mchango
wake mkubwa ambao ameutoa kwa ajili ya kuzisaidia timu 170 za mpira
wilayani Nachingwea na pia kuwawezesha kwa muda mrefu kushiriki katika
michezo ambapo inawasaidia kutokuingia katika matukio ya uhalifu
mitaani. Waziri Chikawe ameanzisha ‘Chikawe CUP’ ambapo kwasasa
mashindano hayo yapo katika ngazi ya Kata mbalimbali ambapo mshindi
atapatikana baada ya kufikia ngazi ya wilaya. Timu ya Ubungo Stars ndio
iliongoza katika mashindano ya Kata ya Namapwia baada ya kuzishinda timu
3 zilizopo katika kata hiyo. Hata hivyo, Chikawe alitoa jezi seti 170
pamoja na mipira 100 kwa ajili ya timu 170 za mpira wa miguu zilizopo
katika jimbo hilo. Picha na Felix Mwagara.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe
(katikati) akiwa katika picha ya pamoja na wachezaji wa timu ya Ubungo
Stars ya Kata ya Namapwia wilayani Nachingwea baada ya timu hiyo kuwa
mshindi wa kwanza baada ya kuzishinda timu tatu zilizopo katika kata
hiyo. Waziri Chikawe aliipa zawadi ya mpira timu hiyo na kuwashauri
wazidi kusongo mbele ili timu hiyo ifike hatua ya Wilaya ili wapewe
zawadi ya Sh500,000 kwa timu itakayonyakua kombe hilo. Hata hivyo,
Waziri Chikawe alitoa jezi seti 170 pamoja na mipira 100 kwa ajili ya
timu 170 za mpira wa miguu zilizopo katika jimbo hilo. Picha zote na Felix Mwagara.
No comments:
Post a Comment