Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Gerald
Guninita, akipokea msaada wa mabati 200, kutoka kwa mwakilishi wa PSPF,
kutoka makao makuu, Amelia Rwemamu, kwa ajili ya ujenzi wa maabara za
sayansi katika shule za sekondari Wilayani humo, Makabidhiano
yalifanyika juzi katika ofisi za Wilaya ya Kilolo
Na Mwandishi wetu.
KATIKA kutekeleza maagizo ya
Rais Jakaya Kikwete, kila shule iwe na maabara tatu ifikapo Novemba mwaka
huu, Mfuko wa Pensheni ya Watumishi wa Umma (PSPSF), umetoa msaada wa
mabati 300 yenye thamani ya zaidi ya Sh Milioni sita, katika Wilaya za
Kilolo na Mufindi, Mkoani Iringa, kufanikisha ujenzi wa maabara hizo na
hosteli kwa Chuo cha Ualimu Mufindi.
Wakati Wilaya ya Kilolo imepata
bati 200 zitakazotumika kusaidia kukamilisha ujenzi wa maabara
unaoendelea katika shule zake za Sekondari, Chuo cha Ualimu
Mufundi (MUTCO), kilichopo Mjini Mafinga Wilayani Mufindi, kimepata bati
100 ikiwa ni kutimiza ahadi iliyotolewa na Meneja wa Sheria wa PSPF,
Abrahamu Siyovelwa, aliyotoa May 27 katika mahafali ya chuo hicho.
Akikabidhi msaada huo kwa mkuu
wa Wilaya ya Mufindi, Monica Kalalu, juzi katika viwanja vya Chuo cha
Ualimu Mufindi (MUTCO), Afisa Mfawidhi wa PSPF Mkoa wa Iringa, Baraka
Jumanne, alisema lengo la msaada huo ni sehemu ya mpango wao katika
kusaidia sekta ya elimu nchini na kutekeleza maombi yaliyoombwa na
viongozi wa Wilaya hizo katika kutekeleza maagizo yaliyotolewa na Rais
Jakaya Mrisho Kikwete, kila shule ya sekondari iwe na maabara ifikapo
Novemba mwaka huu.
“PSPF ni shirika la mfuko wa
pensheni hivyo faida lazima iifikie jamii hasa katika suala la elimu ya
za sekondari na msingi hivyo tumeamua kuwapatia mabati 100 Chuo cha
Mufindi na Wilaya ya Kilolo mabati 200, kutekeleza maombi yao kwa shirika
la PSPF kusaidia ujenzi wa maabara na ujenzi wa hostel kwa chuo cha
MUTCO hivyo leo tunawakabidhi madawati haya mia tatu kwa lengo la
kutekeleza ahadi ya shirika.” Alisema Jumanne.
Aidha Jumanne alitoa wito kwa
viongozi kuwashawishi wafanyakazi Kilolo na wanafunzi wa chuo cha
Ualimu Mufindi kujiunga na mfuko wa pensheni kwa watumishi wa umma (PSPF),
kwa huduma bora na mafao bora yakiwemo mafao ya
uzeeni, ulemavu, mirathi, mafao ya rambirambi za mazishi, malipo ya
wategemezi na malipo ya penshini ya kila mwezi.
Alitoa faida ya kujiunga na PSPF
kwa kuwa kuna baadhi ya mafao mbalimbali yanayotolewa na mfuko huo
yanalenga kuwawezesha watumishi kukabiliana na changamoto mbalimbali
zinazowakabili katika utumishi wao kabla na baada ya kustaafu
Aliongeza kuwa, PSPF ina mpango
imejiwekea mahususi wa kuhakikisha unaboresha maisha wa wanachama wake
wakiwemo wasio wafanyakazi, kwa kuweka akiba isiyo ya hiyari
itakayowawezasha kufaidika kwa faida ya maisha yao.
Kwa upande wake Mkuu wa Milaya
ya Mufindi, Monica Kalalu, alilishukuru shirika la PSPF kwa msaada huo, na
kutoa wito kwa wanafunzi na walimu na kuwataka wadau wengine wajitokeze
kuisaidia sekta ya elimu hususani ujenzi wa maabara ambao unaendelea
nchi nzima kwa sasa,
Naye Mkuu wa Wilaya ya Kilolo,
Gerald Guninita, alisema kuwa msaada huo utazisaidia shule za sekondari
za wilaya ya Kilolo katika kukamilisha ujenzi wa maabara na kuwataka
pspf wasiishie hapo katika kutoa msaada zaidi katika sekta ya elimu.
Na Amelia Rweyimamu ambaye ni
Muwakilishi wa PSPF makao makuu Dar es salaam, akizungumza wakati wa
kukabidhi bati hizo alisema kuwa PSPF inatambua umuhimu wa kuwepo kwa
maabara hapa nchini hivyo ofisi yake imeona vyema kushiri katika ujenzi
huo kwa kutoa bati hizo.
Rweyimamu alisema PSPF inatoa
mafao mbalimbali ikiwa ni pamoja na fao la uzeeni, fao la ulemavu, fao
la kifo, fao la mazishi, fao la wategemezi lisilo na kikomo, fao la
kujitoa, fao la uzee, fao la kufukuzwa kazi, na fao la ujasiriamali.
Aidha aliongeza kuwa PSPF, inatoa
fao la elimu ambapo mfuko hudhamini mikopo katika bodi ya mikopo ya
wanafunzi, lengo kubwa ikiwa ni kujenga uwezo wa kuhudumia wanafunzi
wengi katika taaluma mbalimbali ikiwemo pia taaluma ya sayansi,
Teknolojia na Afya.
No comments:
Post a Comment