Na Mwandishi wetu.
Wanaume wametakiwa kushiriki
katika masuala ya afya ya uzazi, ili waweze kusaidia katika ukoaji wa
maisha ya mama na mtoto wakati wa kujifungua.
Kauli hiyo imetolewa leoJjijini
Dar es salaam na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinisia na Watoto,
Dkt. Pindi Chana, wakati akifungua mkutano wa siku mbili wa Halmashauri
Kuu ya Chama cha Uzazi na Malezi bora Tanzania (UMATI).
Kauli mbiu ya mkutano huo ni miaka 55 ya kutoa huduma bora za uzazi wa mpango Tanzania, ni tumia uzazi wa mpango, okoa maisha.
Amesema katika kusherekea maika 55 ya UMATI, ni vema wadau wote
washirikiane na wataalamu wa sekta ya afya katika kutekeleza kazi
zinatokana na hali halisi ya mahitaji ya huduma ya afya ya uzazi kwa
jamii hususani kwa wanawake, watoto na vijana ili kuokoa maisha ya
wananchi.
Dkt. Chana amesema kuwa, takwimu
kwa Tanzania zinazonyesha kuwa vifo vinavyotokana na uzazi ni takribani
454 kwa kila vizazi hai 100,000 .
Ameongeza kuwa idadi hiyo inaweza kupungua iwapo huduma bora,
taarifa sahihi na elimu kuhusu afya ya uzazi itawafikia Watanzania wengi,
ili liwe taifa lenye uelewa mkubwa kuhusu masuala ya uzazi.
Dkt. Chana ametoa wito kutumia
njia ya makundi rika kama mabaraza ya watoto, vilabu vya watoto na
vyama vya FEMATALK, ili kufikisha ujumbe kwa ajili ya kuokoa maisha ya
mama na mtoto.
Amewataka wajumbe wa mkutano huo
kuendelea na juhudi za kuhamasisha jamii ili kuondoa vitendo vya ubaguzi
wa kijinsia kama vile ndoa za utotoni na wanaume kutoshiriki katika
masuala ya afya ya uzazi sawa na wanawake.
Dkt.Chana ametoa wito kwa UMATI kuendelea na juhudi hizo katika harakati za kumukomboa mtoto wa kike.
No comments:
Post a Comment