KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

October 1, 2014

RAIS DKT. JAKAYA KIKWETE AZINDUA RASMI BARABARA YA MWENGE-TEGETA LEO JIJINI DAR ES SALAA

 

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akihutubia wakati wa ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe jijini Dar es salaam. Ujenzi na upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta Km 12.9, ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete, na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Masaki Okada,  wakifungua kitambaa kuashiria ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe Jijini Dar es salaam. Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Mhe Saidi Meck Sadiki, Mbunge wa Kawe Mhe. Halima Mdee,  na Mwenyekiti wa CCM wa Mkoa wa Dar es salaam, Ndg. Ramadhani Madabida.
Sehemu ya barabara  ya Mwenge-Tegeta yenye urefu wa Km 12.9, ambayo ni sehemu ya mkakati wa Serikali ya Tanzania wa kupunguza msongamano wa magari katika jiji la Dar es Salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Masaki Okada,  wakikata utepe  kuashiria ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe Jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, na Balozi wa Japan nchini Tanzania, Mhe. Masaki Okada,  baada ya ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe Jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, akiongea na Mbunge wa Kawe, Mhe Halima Mdee, baada ya ufunguzi rasmi wa barabara ya Mwenge-Tegeta  leo katika eneo la Lugalo njiapanda ya Kawe Jijini Dar es salaam. PICHA NA IKULU

No comments:

Post a Comment