KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

October 1, 2014

WANACHAMA 75 CHADEMA WAJIUNGA NA ACT

396300_216970381724652_100002350745009_483378_1721045790_n 
 
Na Mwandishi wetu.
 
WANACHAMA 75 kutoka Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kata ya Msasani Jimbo la Kawe, akiwemo Katibu Mwenezi wa Baraza  la Wanawake Chadema Kawe  (BAWACHA), wamejiunga na chama cha Alliance for Change and Transparent (ATC-Tanzania).
 
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa ACT-Tanzania Mkoa wa Dar es Salaam, Khamis Chambuso, wakati akiwakabidhi kadi za chama hicho leo Jijini Dar es Salaam.
 
Chambuso alisema, wanachama hao pamoja na wanachama wengine kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na CHAUMA wamejiunga na ACT- Tanzania kwa mapenzi yao bila kushawishi na kitu chochote.
 
Alisema kwa siku  ya jana wamepokea wanachama 78, ambapo mmoja anatokea Mkoa wa Kigoma na wengine wanatokea mkoa wa Dar es Salaam wengi wao wakiwa ni kutoka CHADEMA.
 
“Kimsingi tunajisikia faraja kuona Watanzania waliowengi wanaanza kutambua umuhimu wetu na wameamua kujiunga na ACT- Tanzania hivyo wanatuongeza nguvu ya kufanya mabadiliko ya nchi”, alisema.
 
Alisema ACT-Tanzania, kina dhamira yua kweli ya kuhakikisha kuwa mfumo mzima wa nchi unabadilika ikiwa ni pamoja na kushirikisha jamii ya Watanzania inafaidika na rasilimali zilizopo hapa nchini.
 
Chambuso alisema ACT- Tanzania haijaja kwa ajili ya kubomoa vyama vingine ila misingi yake ndio chanzo cha watu kutoka vyama mbalimbali kuhitaji kujiunga nao.
 
Mwenyekiti huyo aliwataka wachama hao wapya kuhakikisha kuwa ni sehemu ya mafanikio ya ACT-Tanzania kwa kuongeza wanachama zaidi.
 
Kwa upande wake Mhandisi Mohammed Ngulangwa, ambaye ni Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wa  siku nyingi tangu mwaka 1997, alisema kilichomuondoa CCM ni chama hicho kushindwa kutekeza sera zake.
 
Ngulagwa ambaye mwaka 2010 aliingia katika kinyang’anyiro cha kugombea Ubunge ndani ya chama Jimbo la Temeke alisema kimsingi chama cha ACT-Tanzania ndicho chenye misingi sahihi ya kidemokrasia.
 
Alisema juhudi zake katika siasa atazionyesha kwa nguvu zote ili kuhakikisha kuwa chama hicho kipya kinafanya vizuri katika medani za siasa hapa nchini.

No comments:

Post a Comment