KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

October 21, 2014

RC DAR ALIVYOZINDUA CHANJO YA SURUA NA RUBELLA JIJINI

Wananchi wa Kinondoni na maeneo mengine ya jiji la Dar es Salaam, wakiwa katika uzinduzi wa Chanjo ya Surua na Rubella, Zahanati ya Kambangwa, Kinondoni, Dar es Salaam hivi karibuni
Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Songoro Mnyonge, akimeza dawa wakati wa uzinduzi wa Chanjo ya Surua, Zahanati ya Kambangwa, Kinondoni.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki, akimeza vidonge, wakati akizindua chanjo ya Surua na Rubella, Zahanati ya Kambangwa, Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam juzi. Pia watu wazima walikuwa wakipatiwa dawa za kuzuia Matende na Ngiri maji, wakati wa uzinduzi huo. Chanjo hiyo, iliyoanza juzi itamalizika Oktoba 24, mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki, akipatiwa maelezo na mmoja wa wauguzi wa Zahanati ya Kambangwa, Manispaa ya Kinondoni, Dar es Salaam juzi, wakati akizindua chanjo ya Surua na Rubella.     

No comments:

Post a Comment