UONGOZI wa shule ya Felix Mrema, umejiwekea mikakati ya kutenga kiasi cha Milioni mbili kwa kila mwaka kwa ajili ya kuwapa motisha walimu ambao watawafaulisha vema wanafunzi katika masomo ambayo wanayafundisha shuleni hapo.
Lengo halisi la kutengewa motisha hiyo ni kufanya ushindani wa kufundisha kwa bidii wanafunzi wote madarasani na wakaweza kufaulu kwenye viwango ambavyo vinahitajika hapa nchini.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa shule hiyo, Rashid Nkanga, wakati akiongea na wanafunzi pamoja na walimu wa shule hiyo kwenye maafali ya tano ya kidato cha nne yaliyofanyika shuleni hapo mapema jana.
Rashid alifafanua kuwa, hii ni moja ya mikakati ambayo walibuni na mkakati huo mpaka sasa umeshaweza kuzaa matunda makubwa sana kwani hali ya ufaulu shuleni hapo nayo imeongezeka kwa kiwango kikubwa sana tofauti na hapo awali
“tunajivunia kuona kuwa huu mkakati umezaa matunda makubwa sana hapa shuleni kwani hapo awali hali haikuwa kama ilivyo kwa sasa walimu bora wote wa mwaka wanatangazwa na kupewa tuzo mbele za wazazi kama hamasa ya kuendelea kufundisha kwa bidii zaidi’aliongeza Rashid.
Akionngelea hali ya elimu hapa nchini alisema kuwa ili kiwango cha ufaulu kiweze kuongezeka kwa haraka wakuu wa shule hasa za kata hawana budi kuweka mikakati mbalimbali ambayo itawawezesha walimu wao kufundisha kwa bidii wanafunzi wao
“mimi nadhani kuwa njia mojawapo ya kuendeleza elimu hapa nchini ni kubuni njia na mbinu mbalimbali ambazo zitawafanya hawa walimu wafundishe kwa moyo na mwalimu ambaye amejipinda kufundisha kwa mwaka mzima au mwanafunzi ambaye amesoma kwa bidii kwa mwaka mzima alafu akaja kupewa zwadi mbele ya wenzake atafanya vizuri na yule ambaye alikuwa hafanyi vizuri akiona hivyo ni lazima atafanya vizuri’ aliongeza hivyo.
Alihitimisha kwa kusema kuwa walimu wanatakiwa kufundisha kwa moyo ili kuweza kujenga taifa lenye wasomi kwa hapo baadae lakini kama walimu



No comments:
Post a Comment