KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

October 28, 2014

SHULE YA WAMA NAKAYAMA YAPOKEA MSAADA WA SHILINGI MILIONI 800 KUTOKA UBALOZI WA JAPAN

unnamed
Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Asha  Rose Migoro (kulia), akimkabidhi cheti Kaimu Balozi wa Japan  nchini, Kazuyoshi  Matsu Naga, ikiwa ni ishara ya kutambua  msaada  wa nchi hiyo wa kuisaidia  Shule ya Sekondari ya Wasichana wanaoishi  katika mazingira hatarishi ya WAMA  Nakayama iliyopo katika kijiji cha Nyamisati, Wilayani  Rufiji Mkoani Pwani,   wakati wa sherehe ya mahafali ya pili  ya shule hiyo yaliyofanyika jana.

Na Mwandishi wetu.

UBALOZI wa Japan kupitia Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje, umetoa kiasi cha fedha cha Sh. Milioni 800, ambazo ni sawa na Dola za Kimarekani 500,000 kwa ajili ya kusaidia Shule ya Sekondari ya Wasichana  wanaoishi katika mazingira hatarishi  ya WAMA  Nakayama, iliyopo  wilayani Rufiji  mkoani Pwani.
 
Hayo yalisemwa jana na Kaimu Balozi wa Japan chini,  Kazuyoshi   Matsu  Naga,  wakati  wa sherehe za mahafali ya pili ya shule hiyo, yaliyofanyika jana  na kuhudhuriwa na Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Asha   Rose Migiro, ambaye  alikuwa mgeni  rasmi. Baadhi ya viongozi wakiwemo  baadhi ya wake za viongozi   na wageni wengine mbalimbali.
  
“Juzi Idara ya Mambo ya  nje  ya  Japan, ilikubali kutoa Dola za Marekani 500,000 kwa ajili ya mradi mpya wa awamu ya pili wa kusaidia  shule ya Sekondari ya WAMA   Nakayama,” alisema  Kaimu Balozi huyo.
 
Matsu   Naga aliongeza kwamba, fedha hizo zitatumika kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kompyuta na utawala, yakiwemo mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).
  “Sisi Wajapan,  tunapenda kuendelea kutoa msaada  kadri inavyowezekana. Msaada wa leo utaongeza urafiki kati ya nchi ya Japan na Tanzania,” alisisitiza.
  Kaimu Balozi huyo alimataka kila wanafunzi wa shule hiyo, kutoa mchango wake katika kuleta maendeleo ya jamii kwa kutumia mafunzo aliyoyapata.
 
 Kwa upande wake, Dkt. Migiro, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo, aliwataka  wadau mbalimbali  kuendelea kumsaidia Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Salma  Kikwete,  katika kusaidia wanafunzi hao ili kupanua fursa za watoto wa kike kielimu.
  “Nimegundua kuwa mtoto  wa kike wanakabiliwa na upungufu wa fursa kitaaluma. Hivyo kuchangia shule hii   kwa mtoto  wa kike ni kujenga na kuihimarisha fursa yake  yeye   binafsi na familia kwa ujumla.
  Dkt. Migiro alifurahishwa uweledi wa wanafunzi wa shule hiyo, yakiwemo mazingira bora, ambapo alisema shule hiyo inaviwango bora.
  Naye Mke wa Rais Mama Kikwete, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), aliwataka  wanafunzi hao  kutumia nafasi ya kusoma kwa bidii  ili waweze kufaulu hatimaye  kushika nafasi mbalimbali  za  uongozi kama Dkt.
  Akizungumzia kuhusu matarajio ya WAMA kutokana shule hiyo, alisema kutoa wataalamu wa nyanja zote, ikiwemo fani ya sayansi. Hivyo  aliwataka kuongeza bidii katika masomo ya sayansi.
  Alisema WAMA itaendelea kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu hadi watakapofikia hatua  ya mwisho.
  Waziri  wa Nchi katika Ofisi ya Waziri Mkuu,  Tawala  za Mikoa na Serikali za Mitaa Tamisemi (TAMISEMI), Hawa Ghasia, aliwapongeza walimu wa shule hiyo kwa bidii zao ambazo zimeifanya shule hiyo  kuongoza katika Wilaya hiyo.

No comments:

Post a Comment