KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

October 20, 2014

SIKU YA MSANII KUFANYIKA MLIMANI CITY DAR

12 Ofisa Uhusiano wa Siku ya Msanii Tanzania (SYM), Bw. Peter Mwendapole, akizungumza na Waandishi wa Habari, kuhusu Siku ya Msanii Tanzania, itakayofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City, siku ya tarehe 25 Oktoba, 2014 Jijini Dar es Salaam.

12a 
Mwimbaji wa muziki wa taarabu, Bi.  Isha Ramadhan maarufu kama Mashauzi, akiongea na Waandishi wa Habari kuhusu Siku ya Msanii Tanzania, itakayofanyika katika Ukumbi wa Mlimani City, siku ya tarehe 25 Oktoba, 2014 Jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi wetu

KAMATI ya Siku ya Msanii Tanzania (SYM), imetangaza rasmi majina ya wasanii watakaotumbuiza katika maadhimisho ya siku hiyo, itakayofanyika Oktoba 25 mwaka huu, katika ukumbi wa Mlimani City uliopo Jijini Dar Es Salaam.
 
Akizingumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar Es Salaam, Ofisa Uhusiano wa SYM,  Bw. Peter Mwendapole amesema kuwa, kutokana na siku hiyo kuwa ni ya Sanaa zote, Kamati imeangalia wawakilishi wa sanaa za aina mbalimbali ili ziweze kuwakilisha siku hiyo katika historia ya Tanzania. 
 
“Leo tungependa kuwatangaza Wasanii watatu wa Bendi ya Kilimanjaro Wana Njenje wenye vionjo vya Tanzania na Wawakilishi wa kundi la Wanamuziki wakongwe”, alisema Mwendapole.
 
Mwendapole alisema kuwa, kwa upande wa sanaa kutakuwa na msanii maarufu kama Isha Mashauzi, ambaye atawakilisha fani ya muziki wa jukwaani na upande wa Taarabu, kwani msanii huyo ameweza kufanya mapinduzi makubwa kwenye muziki wa taarabu pamoja na kuweka vionjo mbalimbali vya dansi, asili na taarabu.
 
Aliongeza kuwa, kutakuwa na kikundi cha sanaa kijulikanacho kama Ako Mpiruka Sound, bendi ya muziki, kikundi cha ngoma, kikundi cha sarakasi, wacheza Yoga na pia kutakuwa na shoo ya muziki wa dansi pamoja na dansi za mitaani.
 
Amebainisha kuwa, vijana wanaocheza muziki mitaani wakiwezeshwa wanaweza kujiajiri na kupunguza idadi kubwa ya watu ambao hawana ajira.
 
“Siku ya msanii tunataka kuonyesha jinsi gani wanenguaji wana uwezo wa kucheza bila ya kuonyesha maungo yao”. alisisitiza Mwendapole
 
Akifafanua kuhusu kiingilio cha siku hiyo ya msanii alisema kuwa, kiingilio hicho kitakuwa ni shilingi 70,000 kwa VIP na 50,000 kwa viti vya kawaida.
 
Siku ya msanii inaandaliwa na kampuni Haak Neel Production (T) Ltd, kwa kushirikiana na Baraza la Sanaaa la Taifa (BASATA), na kudhaminiwa na New Habari (2006) LTD, kupitia magazeti ya Bingwa, Dimba, The African, na Mtanzania.
 
Wadhamini wengine wa SYM ni pamoja na PSPF, Azam Media, EFM, Magic FM, Clouds FM, Channel Ten, CXC, Ledger Plaza Hotel na Proin Tanzania.

No comments:

Post a Comment