KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

October 28, 2014

WANANCHI WAASWA KUPITIA KATIBA ILIYOPENDEKEZWA SURA KWA SURA

index
 Na Mwandishi wetu.

WANANCHI   wameshauriwa kuisoma Katiba Mpya Inayopendekezwa  sura kwa sura na ibara kwa ibara, ili waweze kupata uelewa wa masuala mbalimbali yaliyomo ndani ya Katiba hiyo na kuacha kusikiliza maneno  ya watu yenye nia ya kupotosha ukweli.
 
Kauli hiyo ilitolewa jana  na  Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt. Asha   Rose Migiro, wakati  wa sherehe za mahafali ya pili ya Shule ya Sekondari ya Wasichana  wanaoishi katika mazingira hatarishi  ya WAMA  Nakayama, iliyopo  Wilayani Rufiji  Mkoani Pwani.
 
Dkt. Migiro,  ambaye  alikuwa mgeni  rasmi katika sherehe hiyo, ambayo ilihudhuriwa na  baadhi ya viongozi, wakiwemo baadhi ya wake za viongozi  na wageni  wengine mbalimbali.
 
“Nchi yetu ilikuwa katika mchakato wa uandikaji wa Katiba Inayopendekezwa kazi  ambayo ilikamilika Oktoba 8, mwaka huu. 
 
“Tusikubali kusomewa  na tutakapokamilisha kazi ya kuisoma tuipigie kura ya ndiyo,” alisema Dkt. Migiro.
 
Akizungumza na katika mkutano wa mabalozi wanazoziwakilisha nchi zao katika Jamhuri ya Watu wa China uliofanyika kwenye Nyumba ya kufikia Wageni ya Serikali ya Diaoyutai, Beijing, Rais wa Jakaya Kikwete alisema, Kura ya Maoni inatarajiwa  kupigwa wakati wowote Aprili mwaka ujao kama mambo yataenda vizuri.
 
Rais Kikwete alikabidhiwa Katiba hiyo hivi karibuni mjini Dodoma, baada ya Bunge Maalum la Katiba kumalizia kaze yake.

No comments:

Post a Comment