KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

November 1, 2014

BARAZA LA MADIWANI LAITAKA REA KUFIKISHA UMEME VIJIJINI KWA WAKATI

indexNa Mwandishi wetu.

BARAZA la madiwani wa Halmashauri ya Arusha, limemtaka Wakala wa Usambazaji wa Umeme Vijijini (REA), kuhakikisha kuwa vijiji vyote vilivyoko kwenye mpango wa kupatiwa umeme vinapata kwa wakati kwani kwa sasa mashimo yalichimbwa yanahatarisha maisha ya wananchi.

Mbali na baraza hilo kuwataka REA kufikisha umeme kwa wakati vijijini, lakini pia wanatakiwa kuifanya jamii iweze kuwakubali tofauti na sasa ambapo wamechimba mashimo ya kusimamamishia nguzo na wameyaacha.

Akiongea na katika Baraza hilo la Madiwani lililofanyika jana, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Saimon Saningo, alisema  kuwa ni muda mrefu sasa umepita toka wakala hao wachimbe mashimo na kuyaacha kama yalivyo jambo ambalo limewafanya wananchi kubaki na malalamiko.

Amedai kuwa, mashimo hayo yanahatarisha sana maisha ya wananchi, lakini pia hata mifugo ambayo ipo vijijini humo na kwa hali hiyo wananchi wamebaki wakiwa na manung'uniko makubwa.
  Ameongeza kuwa, endapo kama muda wa kufikisha umeme vijijini haujafika, basi REA wanatakiwa kwenda kufukia mashimo hayo na pindi watakapokuwatayari basi watayafukua na kisha kusimamisha nguzo kwa ajili ya umeme.

Hata hivyo, ameitaka  REA kuhakikisha kuwa wanashirikiana na madiwani waliopo kwenye Kata husika, kwani takwimu za halmashauri hiyo zinaonesha kuwa bado asilimia kubwa ya madiwani hawajui mradi huo.

Amesema  kuwa, wakati mwingine wananchi wanashindwa kupenda na kuthamini mradi huo kwa kuwa hawana hamasa kutoka kwa madiwani hao, hali ambayo wakati mwingine inasababisha fujo zisizo za lazima hasa maeneo ambayo mradi huo umepita.

No comments:

Post a Comment