KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

November 29, 2014

BUNGE LASAMBARATIKA TZ

Mzozo mkubwa umesababisha Bunge la Tanzania kuvunjika usiku wa jana wakati likiendelea na mjadala wa kashfa ya Escrow, baada ya wabunge kushindwa kukubaliana njia sahihi ya kuwawajibisha baadhi ya viongozi wa kisiasa wanaotuhumiwa kuhusika na sakata la wizi wa Zaidi ya fedha za Tanzania shilingi bilioni 300 kutoka Benki Kuu ya nchi hiyo.
Taarifa ya mwandishi wa BBC Baruan Muhuza imesema kuwa Bunge hilo, jana limeweka rekodi ya kuwa na mjadala wa muda mrefu Zaidi kuliko wakati mwingine wowote. Hadi kufikia kuvunjika kwa kikao hicho ilikuwa ni saa 4.30 usiku kwa saa za Afrika Mashariki. Spika wa Bunge hilo Anne Makinda karibu muda wote wa kikao hicho alijikuta akitoa tahadhari kwa wabunge wake kujilinda na hatua za kuingilia mihimili mingine ya utawala ya Tanzania ambayo ni Mahakama na Serikali. Hatua hiyo kwa namna fulani iliamsha hisia tofauti kutoka upande wa kambi ya upinzani pamoja na wajumbe wa kamati ya hesabu za Serikali ambao walitishia kutoka nje hadi viongozi wanaodaiwa kulindwa na bunge hilo wawajibike wenyewe. Bunge hilo linategemewa kuendelea na kikao chake hapo leo.

No comments:

Post a Comment