KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

November 24, 2014

COMRADE KINANA AANZA ZIARA MKOANI, AKUTANA NA VIONGOZI WA SUDAN KUSINI


23
Katibu Mkuu wa CCM, Ndg.  Abdulrahman Kinana akinyanyua mikono juu kuashiria mshikamano na baadhi ya viongozi wa makundi ya Chama cha SPLM cha Sudan Kusini ambao wako kwenye mgogoro wa kugombea madaraka kwa takribani mwaka sasa. Kinana amekutana na viongozi hao wakati wa mkutano wa hadhara mjini Masasi, Mtwara baada ya kumfuata na  kutaka ushauri wa upatanishi nchini kwao  Sudani Kusini. Baada  ya viongozi hao kupata wasaa wa kusalimiana na  wananchi katika mkutano huo uliofanyika mjini Masasi Baadae Kinana  alifanya nao mazungumzo Ikulu Ndogo ya Masasi. Viongozi hao wamemfuata Kinana mjini Masasi kutokana na kwamba yuko katika ziara  ya kikazi ya mikoa ya Lindi na Mtwara akiendelea na shughuli za kuimarisha Chama hicho na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 akiongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi
 20
Viongozi wa vikundi hivyo wakiwa mjini katika mkutano wa CCM mjini Masasi
1c
Kinana akizungumza na viongozi hao ikulu ndogo mjini Masasi
1
Katika ziara yake inayoendelea mkoani Mtwara Kinana alitembelea kiwanda cha kubangua korosho na kujieonea shughuli mbalimbali  zinazofanywa kiwandani hapo hapa akionyesha wa mashine ya kufunga korosho.
3
Baadhi ya akina mama wafanya kazi wa kiwanda hicho wakichambua korosho na kuzitenga katika madaraja
4
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia mashine za kisasa za kubangua korosho
5
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza baada ya kukagua kiwanda hicho kinachomilikiwa na mama Kate Kamba. kulia
7
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Afisa Ushirika wa Mkoa wa Mtwara Bw. John Henjewele kuhusu matatizo ya korosho kushoto ni Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi, Siasa na Uenezi.
8
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa Makaravati katika barabara ya Migongo mjini Masasi

No comments:

Post a Comment