KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

November 23, 2014

SOTE TULAANI UKATILI HUU WA HOUSE GIRL WA UGANDA

Sote inapaswa tuaani kitendo alichokifanya msichana wa ndani wa Uganda Jolly Tumuhirwe (22) cha kumsigina na kumpiga mtoto wakati akimnywesha uji.

Inasemekana mtoto alikuwa anaumwa na hivyo hakuwa na hamu ya kula. Baba wa mtoto anaitwa Erick kamanzi na wakati ukatili huo unafanyika hakuwepo ila kilichomfanya ajue yote hayo ni kamera aliyoitegesha sebuleni kwa siri.

Alivyorudi nyumbani alimkuta mtoto akiwa na michubuko na alichokifanya ni kupitia mkanda wa kamera yake kazi ambayo ilichukua muda kidogo.

Baada ya kuperuzi kamera hiyo na kuona kilichotokea mara moja alimrarua yule house girl mithili ya chui, yule dada (Jolly) kuona hivyo akakimbilia polisi na kudai kwamba bosi wake anataka kumuua.

BOSI AKAMATWA

Polisi walimkatama  Kamanzi na kumuweka rumande,alipopoa hasira akiwa rumande aliwanyesha polisi mkanda wa kamera yake na ndipo polisi walipogeuza kibao na kumshitaki Jolly kwa makosa ya utesaji na sasa wanataka kuyageuza makosa hayo kuwa ya kudhamiria kuua . Haijajulikana kwanini mama wa mtoto huyo anayeitwa Angella haishi na mototo huyo.Angella ni Mnyarwanda.


Kwasababu ya kulinda haki za mtoto pamoja na sheria zinazofuatwa na Google hatutaweza kuwaonyesha video hiyo. SOTE TUNAPASWA TULAANI UKATILI HUO
Kamanzi (L) and his kids. Right is the tortured baby

No comments:

Post a Comment