KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

November 26, 2014

MAHAKAMA YALIPIGA 'STOP' BUNGE KUJADILI KASHFA YA ESCROW LEO


 
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imelizuia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kujadili suala la akaunti ya Escrow mpaka kesi ya msingi iliyofunguliwa na IPTL itakapojadiliwa.

Kwa mujibu wa chanzo chetu,mteja IPTL alikwenda mahakamani hapo kutaka ufafanuzi wa vipengele kadhaa vya kisheria ikiwamo uhalali wa Mkaguzi Mkuu wa Serikali kuikagua kampuni hiyo wakati tayari mahakama ilishatolea maamuzi suala la mahesabu ya kampuni hiyo.

Vigogo kadhaa wanatuhumiwa kuchota fedha zaidi ya sh. bilioni 300 katika akaunti ya Tegeta Escrow ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT),na hatma yao ingejulikana leo wakati ripoti ya uchunguzi wa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), ingewasilishwa na kujadiliwa bungeni hapo,

Hatua hiyo ni baada ya Bunge kutuliza munkari wa wabunge hao wiki iliyopita kwa kuthibitisha kwamba hakuna barua yoyote iliyowasilishwa na Jaji Mkuu ili kuzima mjadala wa ripoti hiyo kama ambavyo imekuwa ikidaiwa.

Kauli hiyo ilitolewa hivi karibuni na Mwenyekiti wa Bunge, Mussa Hassan Zungu, wakati akitoa mwongozo wake kuhusu madai kwamba Mahakama imeandika barua kwenda ofisi ya Spika kuzuia mjadala wa kashfa ya IPTL.

No comments:

Post a Comment