KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

November 26, 2014

TAHADHALI KWA WANAWAKE WA JIJINI DAR,WATAKIWA KUTOSHIRIKI MAPENZI NA WATU WASIOWAJUA



Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam linatoa tahadhari kwa wanawake wa jiji la Dar es Salaa hususani wasichana kuwa makini na wanaume wanaowataka kimapenzi na baadaye kuwauwa na kutelekeza miili yao.

Zimekuwepo taarifa juu ya kuwepo kwa wanaume wawili wanaoshawishi wanawake kuwa nao kimapenzi na baada ya muda huwauwa. Hivyo natoa tahadhari kwa wanawake wa jiji la Dar es Salaam kuchukua tahadhali juu ya watu hawa maana huatarisha maisha yao au ya familia zao.

Inaaminika watu hao huwashawishi akina dada au wanawake kwa jumla ili wawe nao kimapenzi huku wakiwasaidia kwa huduma mbalimbali za kimaisha na kisha kuwauwa.

Natoa wito kwa wanawake wote kutokukubali kushawishiwa kirahisi na wanaume wasiowajua ambao wanataka kuwa nao kimapenzi na starehe kwani kwa kufanya hivyo wanaweza kuingia katika mtego mbaya na pengine hata kuyaweka maisha yao rehani.Anasema Kamanda Suleiman Kova,bosi wa Polisi Jijini Dar.

No comments:

Post a Comment