KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

November 29, 2014

RAIS KIKWETE KUREJEA NCHINI LEO, JE KITENDAWILI CHA ADHABU YA WATUHUMIWA WA UFISADI ATAKITEGUA?

Jakaya-Kikwete
Dkt Jakaya Kikwete                                                                                                              Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwasili leo nchini akitokea Marekani ambako alikuwa anatibiwa kwa siku kadhaa. Rais anawasili huku kuwa na sintofahamu juu ya hatua za kuchukua dhidi ya watuhumiwa wa muamala wa fedha za Escrow. Picha iliyoonekana jana katika kikao cha Bunge inaonyesha kwamba serikali bado inakigugumizi juu ya kuwachukulia hatua viongozi wake waandamizi wanaotuhumiwa kuucheza mchezo huo mchafu. Wadadisi wa mambo wanasema kuwasili kwa Rais kunaweza kukuwa ni jawabu la tuhuma hizo za ufisadi.Wanadai kwamba uimara wa chama tawala CCM kunategemea maamuzi yatakayolewa na kuhusiana na kadhia hiyo mbaya. Hivyo basi ni wazi maamuzi hayo yatakayotolewa dhidi ya watuhumiwa yataonyesha picha ya baadaye itakayokuwa nayo chama tawala. Wananchi wengi hawependi namna ambavyo Bunge la wana CCM wengi linataka kuwalinda watuhumiwa wa ufisadi hasa ikizingatiwa maisha sasa ni magumu.


No comments:

Post a Comment