KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

November 26, 2014

WARIOBA MIMI NI MWANA CCM JAPO NAJUA KUNA WANA CCM MASLAHI NA CCM IMANI

Image result for warioba image
ALIYEKUWA Mweyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba ,Jaji Mstaafu na Waziri Mkuu Mstaafu Joseph Sinde Warioba amesema kwamba yeye hawezi kuhamia upinzani na kwamba atabaki kuwa mwana CCM tu.
"Najua sasa hivi kuna wana CCM imani na wana CCM maslahi, mimi siwezi kwenda upande wa pili nitabaki CCM ," alisema jana huku akishangiliwa.
Akizungumza katika kongamano la jana la Katiba, Mlimani City Jijini Dar es Salaam, aliwashauri vijana kuielewa katiba iliyopitishwa na Bunge Maalum la Katiba maana ni katiba yao na ya watoto wao na vizazi vijavyo.
"Kazi yangu ni kuwashauri muijue, ili muweze kuamua kwa busara," kuhusu swali la kijana mmoja kwamba wafanyaje sasa baada ya katiba ile kupita, akasema bado kuna safari ndefu, ila wajifunze katiba hiyo na waamue maamuzi ya maana kwa maslahi ya nchi yetu kwa amani kabisa. 

No comments:

Post a Comment