Tigo imetangaza leo kwamba imetoa malipo yake ya
kwanza ya kila robo mwaka ya kiasi cha shilingi bilioni 3 (dola milioni
1.8) kwa wateja wake wa Tigo Pesa. Mgao huu ni wa kwanza kati ya awamu
nne za malipo zinazotarajiwa kufanyika kila mwaka.
Malipo haya yanafanyka miezi mitatu baada ya kampuni hiyo kulipa
kiasi cha shilingi bilioni 14.25 (dola milioni 8.64) ambacho kilikuwa
kimelimbikizwa katika mfuko wa fedha ya akaunti ya Tigo Pesa, malipo
yaliyoifanya Tigo kuwa kampuni ya simu ya kwanza duniani kuwagawia faida
watumiaji wake wa huduma ya fedha kwa simu za mkononi. Tigo Pesa ina
jumla ya watumiaji milioni 3.6.
Meneja Mkuu wa Tigo Diego Gutierrez alisema, “Hii duru ya pili
ya kutoa gawio ni udhihirisho tosha wa muendelezo wa kampuni yetu katika
kuwanufaisha wateja na kuboresha maisha ya Watanzania. Malipo haya
yanaenda kwa kila mtumiaji wa Tigo pesa wakiwemo mawakala wakuu,
mawakala wa reja reja na watumiaji wa kawaida wa huduma hii. ”
“Gawio la kwanza lilikuwa kubwa zaidi kwa sababu faida
ilimbikizwa kwa muda wa zaidi ya miaka mitatu na nusu ikilinganishwa na
malipo haya ya pili ambayo yanatokana na malimbikizo ya faida ya fedha
zilizohifadhiwa katika mifuko ya benki za kibiashara kwa muda wa miezi
mitatu t kutoka Julai hadi Septemba 2014,” alisema Meneja Mkuu huyo.
Gutierrez alieleza kwamba, kama ilivyokuwa hapo awali, malipo
wanayopata wateja awamu hii yanatokana na salio lao la kila siku kwenye
akaunti zao za Tigo Pesa. Hii ni kwa wote; mawakala wakuu, mawakala wa
reja reja na watumiaji wa kawaida.
Mgao unaofuata wa mwezi Oktoba mpaka Desemba 2014 utalipwa mwezi Februari 2015.
Kuhusu Tigo:
Tigo Tanzania ni kampuni ya mawasiliano inayoongoza kwa ubunifu
nchini, inafahamika kama kampuni inayolenga kuleta maisha ya kidijitali
katika jamii. Inatoa huduma tofauti tofauti za mawaliano kwa njia ya
simu, intanet ya kasi na kutuma na kupokea fedha. Aidha Tigo imebuni
bidhaa na huduma mbali mbali kama Facebook kwa Kiswahili, Tigo Pesa App
kwa watumiaji wa simu za Android na iOS, na ni kampuni ya simu ya kwanza
Afrika Mashariki kuanzisha huduma ya kutuma na kupokea pesa kwa njia ya
simu kimataifa, yenye uwezo wa kubadilisha fedha za kigeni.
Kwa kutumia tekinolojia ya 3G Tigo ina wahakikisha wateja
upatikanaji wa huduma bora na za uhakika. Kati ya mwaka 2013 na 2014,
kampuni ilizindua minara mipya zaidi ya 500 na pia ina mipango wa
kuongeza mara mbili kiwango cha uwekezaji ifikapo mwaka 2017 ili kuweza
kupanua wigo wa mawasiliano na uwezo wa mtandao hasa hasa katika maeneo
ya vijijini. Tigo ina wateja zaidi ya milioni 7 na inatoa ajira za moja
kwa moja na kwa namna mbali mbali kwa Watanzania zaidi ya 100,000 ambao
wanajumuisha wafanyakazi wa huduma kwa wateja, wa kutuma na kupokea
fedha, watu wa mauzo pamoja na wasambazaji.
Tigo ni kampuni ya simu inayoongoza chini ya kampuni mama ya
mawasiliano Millicom, ambayo imejizatiti katika kuhamasisha na
kufanikisha maisha ya kidijitali katika nchi 44 zenye biashara zake
Afrika na Latin Amerika, pamoja na ofisi za kampuni zilizopo Ulaya na
Marekani. Kwa kutambua kwamba ubunifu ndio utakaowafanya kuendelea kuwa
juu ya ushindani, Millicom inaendelea kuthamini mchango wa wadau wake,
wakitumia dhana ya “demand more” kama namna ya kufanya biashara na
kuendeleza nafasi yao kama kampuni inayoongoza katika kufanikisha maisha
ya kidijitali katika baadhi ya masoko makubwa yenye ushindani mkali
duniani.
No comments:
Post a Comment