KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

November 26, 2014

WATU WANNE AKIWAMO POLISI JELA MIAKA 120


MAHAKAMA ya Wilaya ya Mbeya imewahukumu kifungo cha miaka 120 watu wanne akiwemo aliyekuwa askari wa jeshi la Polisi baada ya kukutwa na hatia ya unyang’anyi wa kutumia silaha.
Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Mbeya, James Mhanusi,ambapo  mbali na kuwatia hatiani washitakiwa hao Mahakama hiyo pia imemuachia huru mshtakiwa mmoja kwa kile kilichoelezwa kuwa hakuna ushahidi unaomhusisha na tukio moja kwa moja.
Mwendesha mashtaka wa Serikali,Catherine Paul, aliwataja washtakiwa kuwa ni aliyekuwa Askari wa Jeshi la Polisi,8303 Pc James, Elinazi Mshana,Lusajo Jeremia na Abdalah Mohamed ambao kwa pamoja walitenda kosa la unyang’anyi wa kutumia silaha Oktoba 7, 2013.
Mwendesha mashtaka huyo alisema watuhumiwa hao wenye kesi namba 23/2014 walitenda kosa hilo kinyume cha kifungu cha 287 (a) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 ambapo walifanikiwa kupora Kahawa yenye thamani ya shilingi Milioni 119.2 yenye uzito wa kilogramu 30091.
Akisoma Hukumu kwa watuhumiwa hao, Hakimu Mhanusi amesema kutokana na ushahidi wa upande wa mashtaka na upande wa utetezi mahakama imeona mshtakiwa namba tatu katika kesi hiyo ambaye ni Gwantwa Malakasuka hakukuwa na ushahidi unaomtia hatiani pasipo shaka hivyo akaamuru kuachiwa huru.
Kwa upande wa Washtakiwa wengine, amesema ushahidi wa mazingira pamoja na kutambuliwa na shahidi wa kwanza ambaye pia ndiye aliyekuwepo eneo la tukio unathibitisha pasipo shaka kutenda tukio hilo kutokana na kufanya tukio hilo majira ya jioni wakati kuna mwanga hivyo ilikuwa rahisi kutambuliwa.

No comments:

Post a Comment