KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

December 23, 2014

BREAKING NEWS-VURUGU KUBWA ZAZUKA KARIAKOO




HABARI zilizotufikia muda huu zinasema vurugu kubwa zimezuka eneo la Kariakoo Jijini Dar es Salaam na kusababisha Jeshi la Polisi kurusha risasi hewani  ili kuwatawanya wafanyabiashara ndogondogo (wamachinga) ambao inadaiwa walianzisha vurugu hizo.
Chanzo chetu kinasema  barabara za kuingia na kutoka Kariakoo zilifunwga kwa muda kutokana na wamachinga hao kuchoma magurudumu  ya magari barabarani .
Chanzo hicho kinasema chanzo cha vurugu hizo ni madai ya kuuawa kwa mwenzao(machinga)  na mgambo wa Jiji.
Chanzo kinasema mfanyabiashara huyo anadaiwa kuuwawa na mgambo hao kwa kipigo.Wanadai kuchoshwa na manyanyaso hayo hali ambayo imewafanya kujichukulia sheria mkononi. Ni kinyume na sheria za nchi kujichukulia sheria mkononi . Wanadai kuwa walifanya vurugu hizo ili kuonyesha hisia zao kwa serikali juu ya suala hilo. KWA HISANI YA FULL HABARI BLOG

No comments:

Post a Comment