Ujumbe wa wataalamu wa Mamlaka ya
Bandari Tanzania ( TPA) unatembelea Bandari ya Singapore (PSA) ili
kubadilishana utaalamu wa namna ha kuongeza ufanisi na kuimarisha Ulinzi
na usalama wa Bandari kwa kutumia Mitambo ya kisasa na Teknolojia ya
Habari na mawasiliano (ICT) , Ujumbe wa TPA unaongozwa na Ndg. Phares
Magesa , Mkurugenzi wa ICT wa TPA, pia wamo wahandisi wa majengo,
wataalamu wa Ulinzi na wataalamu wa TEHAMA. Ziara hii ni muendelezo wa
ushirikiano wa PSA na TPA ikiwa ni sehemu ya makubaliano yaliyotiwa
sahihi kati ya TPA na PSA wakati wa ziara ya Mhe. Rais Kikwete
alipotembelea nchini Singapore mwaka jana.Mkuu
wa msafara wa TPA Ndg. Magesa akipokea zawadi toka Makamu wa Rais
Msaidizi wa Mamlaka ya Bandari ya Singapore ( PSA) anayeshugulikia
biashara Ndg. Vignes kulia
Mkuu
wa msafara Ndg. Magesa akisalimiana na Makamu wa Rais Msaidizi wa PSA
anayeshugulikia ICT Ndg. Andrew Gill wakati akiwakaribisha makao makuu
wa PSA Ujumbe wa TPA ukiwa kwenye mazungumzo na Ujumbe wa PSA makao makuu ya PSA
No comments:
Post a Comment