Gari la kivita la Serikali nchini Misri
Takriban watu 26 wameuawa katika
mfululizo wa mashambulizi yaliyofanywa na kundi la wapiganaji la Islamic
State Kaskazini mwa Misri katika eneo Sinai
Gari lililokuwa na
mabomu lilipiga kituo cha kijeshi kaskazini mwa Sinai katika mji wa
El-Arish na kuwaua wanajeshi kadhaa. Mashambulizi mengine kama hayo
yalifanyika katika mji jirani Sheik Zuwayid na mji wa Rafah katika mpaka
wa Gaza.
Kundi la wapiganaji la Ansar Beit al-Maqdis ambalo ni
mshirika wa wapiganaji wa Islamic State wamekiri kutekeleza shambulio
hilo.
Maafisa wa jeshi nchini Misri wanasema gari hilo lililokuwa
na mabomu liliegeshwa nje ya ngome ya jeshi ya El-Arish na mashambulizi
yake yalilenga hoteli ya jeshi na maeneo mengine mhimu katika kituo
hicho.
Hata hivyo kundi hilo lilianza kutekeleza mashambulizi yake
nchini Misri tangu kuangushwa kwa utawala wa Rais aliyekuwa na msimamo
mkali wa Kiislam Mohammed Morsi mwaka 2013.
Hofu imetawala katika
miji kadhaa nchini Misri wiki hii kutokana na sherehe za kumbukumbu za
kuangushwa kwa utawala wa aliyekuwa Rais wa Taifa hilo na aliyeondolewa
madarakani mwaka 2011 Hosni Mubarak -BBC


No comments:
Post a Comment