| Pichani ni Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahimu Lipumba picha na Maktaba |
UMOJA wa
Kutetea katiba ya Wananchi UKAWA umesema utasusia zoezi la upigaji wa
kura wa Katiba iliyopendekezwa na Bunge Maalum la katiba inayotarajiwa
kupigwa mwezi wa nne mwaka huu kwa Madai Rais Jakaya Kikwete amekiuka
makubaliano na Vyama vya siasa waliokubaliana mwaka jana mjini Dodoma
.Na KAROLI VINSENT anaripoti. Endelea nayo.
Azimio hilo limetangazwa jana Jijini Dar Es Salaam na Mwenyekiti
mwenza wa Umoja wa vyama Vikuu vya Upinzani vinavyounda Umoja wa
kutetea Katiba ya Wananchi UKAWA Freeman Mbowe, wakati wa mkutano na
Waandishi wa habari ambapo amesema Umoja huo hauwezi kuwepo katika
mipango ya kuingamizi nchi wakati wa kupitisha katiba isiyokuwa na
chembe yeyote ya kumsaidia mtanzania.
“Tunasema
kwa pamoja hatutoshiriki katika katika kura za wa kupitisha katiba ya
chama cha Mapinduzi,katiba iliyotengenezwa bila ya kuwa na maridhiano ya
Kisiasa,maana Rais Kikwete ameamua kwa makusudi kabisa kutusaliti sisi
viongozi wenzake wa kisiasa,tulikubaliana kwamba Bunge lile lisitishwe
kutokana na kutoweza kupatikana kwa katiba mpya lakini alivyotoka pale
akatusaliti na kuendelea na Bunge lile lilotafuna pesa za wananchi
walalahoi”alisema mbowe.
Mbowe aliongeza kuwa katika makubaliano hayo walifikia maazimio ya
kufanyia mabadiliko katiba iliyopo ya mwaka 1977 katika vipengele
mbalimbali ikiwemo kipengele cha kuwepo tume huru ya uchaguzi lakini
Rais Kikwete akawageuka dakika za mwisho.
Mbowe ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Hai alizidi kusema kwa uchangu kwamba
Umoja huo umebaini rafu mbalimbali wananazozifanya Chama cha mapinduzi
ili katiba iliyopendekezwa iwe katiba harala kwa kuwasafirisha watu
kutoka Mkoa wa dare s Salaam hadi Visiwani Unguja na pemba ili wakati wa
kupiga kura ya kupitisha katika Iliopendekwa na bunge waipigie kura ya
Ndio ambapo mbowe anasema wao hawatakubali.
vyama hivvyo Vinavounda UKAWA ni CUF,Chadema,NCCR mageuzi na NLD
Kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha NLD Dk.
Emmanuel Makaidi amesema chama chake kitazunguka nchi nzima kuhamisha
wananchi kutopigia kura katiba pendekezwa kwa Madai Katiba hiyo
inamapungufu kibao na itazidi kuwaweka katika mazingira magumu yenye
kujaa umasikini.
Naye Mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi James Mbatia alisema
anashangaa kitendo cha Rais Kikwete kuwageuka na kuyatupia mbali
makubaliano yao waliosema mchakato usitishwe mpaka baada ya uchaguzi
mkuu na kufanyia marekebisho ya Katiba iliyopo na kusema kitendo hicho
kinaonyesha kiongozi huyo alivyokuwa kigeugeu na umoja huo hautokubali.
Vilevile Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahimu Lipumba
alisema Katiba wanayoitaka kuipitisha kinguvu haina mshiko kwa
watanzania na imekaa kwa ajili ya kuwanafaisha watawala walioko
madarakani,na akasema chama chake hakitokubali kuwepo katika dhambi ya
kuwahujumu wa Tanzania na wao watasusia mchakato huo.


No comments:
Post a Comment