
WAZIRI
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amejiuzulu nafasi yake baada ya
kile alichosema ni kuandamwa kila kona kuhusu sakata la Akaunti ya Escrow huku
akisisitiza kuwa yeye hahusiki hata kidogo na kashfa hiyo.Akizungumza na waandishi wa habari mda mfupi uliopita, Profesa Muhongo
alisema ameamua kuchukua uamuzi huo baada ya kushauriana kwa kina na Rais
Jakaya Kikwete pamoja na familia yake.Amesema kashfa ya Escrow imemdhalilisha yeye na familia yake ilhali
hahusiki na kumtaka mtanzania yeyote mwenye ushahidi aupeleke mahakamani ili
sheria ichukue mkondo wake.
Ametaja sababu nyingine ya kujiuzulu kwake kuwa ni kukisaidia chama
chake (CCM), ili kurudisha imani ya wananchi kwa chama hicho na serikali kwa
ujumla kutokana na kuadhibiwa chama badala yake.Kujiuzulu kwa Profesa Muhongo yumkini kukakamilisha tamthiliya ndefu ya
kashfa ya Escrow kwa kuwa watuhumiwa wote wa sakata hilo waliopendekezwa na
bunge wamewajibishwa au kuwajibika.Sakata la Akaunti ya Escrow lilisababisha kujiuzulu kwa Mwanasheria Mkuu
wa serikali, Fredirick Werema kwa kushindwa kuishauri vizuri serikali kuhusu
fedha za akaunti hiyio, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa
Anna Tibaijukana kutokana na kupokea mgao wa fedha hizo, pamoja na wenyeviti wa
kamati za Bunge Andrew Chenge, Victor Mwambalaswa na Wiliam Ngeleja pia kwa
kupokea mgao wa fedha hizo.
![]() |
| Alivyokuwa ana bwaaga manyanga |
![]() |
| Sehemu ya wanahabari waliohudhuria mkutano huo wa kubwaga manyanga |




No comments:
Post a Comment