KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali na Mashirika ya Umma (PAC),
imeagizwa kufikishwa mahakamani kwa watumishi wa Shirika la Ndege la
Tanzania (ATCL) waliohusika na mkataba wa ukodishaji ndege mbovu.
Akizungumza wakati wa kuhitimisha taarifa ya PAC kwenye kikao
kilichopokea taarifa ya ATCL, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Zitto Kabwe,
alisema ukodishwaji wa ndege kutoka Kampuni ya Wallis Trading Inc. ya
China kulikofanywa na wataalamu wa Tanzania kuliisababishia serikali
deni la dola milioni 42.4.
Alisema hadi sasa waliofanya madudu hayo hawajachukuliwa hatua,
wakati serikali inalipa hasara hiyo kuanzia Oktoba mwaka jana na kwamba
hadi sasa imekwishalipa dola milioni 26.1.
“Utaratibu huu wa kuwaacha watu wanaohujumu waendelee na utumishi
serikalimi haufai kwa sababu watakuwa wanafuja fedha za umma wakijua
hakuna hatua yoyote itakayochukuliwa dhidi yao,” alisema Zitto.
Akirejea historia ya tukio hilo, alisema Kampuni ya Wallis ilisaini
mkataba na ATCL Oktoba 2007 wa ukodishwaji wa ndege kwa kipindi cha
miaka sita kwa malipo ya dola 370,000 kila mwezi, ikiwa ni gharama za
kukodi ndege na Serikali iliridhia kutoa dhamana.
Alisema baada ya ndege kuwasili ilifanya kazi kwa kipindi cha miezi
sita tu na ilipofika Desemba 2008, Mamlaka ya Usafiri wa Anga iliifungia
ATCL kwa kushindwa kutekeleza matakwa ya usafiri wa anga, ikiwemo
kurekebisha vitabu vinavyoeleza mambo ya usalama wa ndege.
Alisema ndege hiyo ilipelekwa Mauritania kwa ajili ya matengenezo ya
kawaida mwezi Machi mwaka 2009 na ilipofika Julai 2009 ilipelekwa
Ufaransa kwa ajili ya matengenezo makubwa baada ya kutimiza miaka 12
tangu ilipotengenezwa kwa mujibu wa taratibu za matengenezo ya ndege.
Zitto alisema mkataba wa ukodishwaji na matengenezo yote yalipaswa
kufanywa na ATCL, lakini kwa sababu ya hali mbaya ya kifedha ya
serikali, ndege hiyo ilishikiliwa na aliyeifanyia matengenezo hadi
mkataba wa ukodishwaji ulipovunjwa Oktoba 11 mwaka 2011.
“Mbaya zaidi Wallis alimwandikia Mwanasheria Mkuu wa Serikali
kumweleza nia ya kutaka kuishtaki Serikali kwa kushindwa kulipa deni
hili.



No comments:
Post a Comment