![]() |
| Katibu Mkuu Kiongozi,Ba;ozi Ombeni Sefue akitangaza mabadiliko hayo mbele ya Waandishi wa Habari Jijini leo |
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amefanya mabadiliko kwenye Baraza la Mawaziri leo.
Akitangaza mabadiliko hayo Katibu Mkuu Kiongozi Ofisi ya Rais, Balozi Ombeni Sefue aliwataja Mawaziri hao wapya ambao
wanaapishwa jioni hii na Wizara zao kwenye mabano kuwa George
Simbachawene (Nishati na Madini), Mary Nagu (Mahusiano na Uratibu), Dk.
Harrison Mwakyembe, (Afrika Mashariki).
Wengine ni Wiliam Lukuvi (Ardhi, Nyumba na Makazi), Steven Wassira
(Kilimo Chakula na Ushirika), Samwel Sitta (Uchukuzi), Jenista Mhagama
(Sera na Uratibu wa Bunge) na Christopher Chiza (Ofisi ya Waziri Mkuu
Uwekezaji na Uwezeshaji).
Rais pia ameteua Manaibu Waziri na Wizara zao kwenye mabano kama
ifuatavyo: Steven Masele (Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano), Angellah
Kairuki (Ardhi Nyumba na Makazi), Ummy Mwalimu (Katiba na Sheria), Anna
Kilango Malecela (Elimu na Mafunzo ya Ufundi), Charles Mwijage (Nishati
na Madini).



No comments:
Post a Comment