Mhambuliaji Mbwana Samatta.
Na Mwandishi Wetu
MSHAMBULIAJI Mbwana Samatta sasa anarejea nchini DR Congo kuendelea kuichezea klabu yake ya TP Mazembe, akionekana kama shujaa kutokana na kufaulu licha ya kushindwa kuchukuliwa kucheza Ulaya.
Samatta alifanya majaribio katika kikosi cha CSKA Moscow cha Russia ambacho kilikuwa kimeweka kambi nchini Hispania.Meneja wa Mbwana Samatta, Jamal Kisongo amesema baada ya kufanya majaribio, CSKA ilikubali kumchukua kwa mkopo lakini tatizo likawa ni mawasiliano.
“Amefanya majaribio vizuri kabisa, lakini tatizo likawa kubwa katika suala la mawasiliano. CSKA Moscow ilikuwa inamtaka kwa mkopo. “Lakini Mbwana hawezi kuondoka bila ya ruhusa ya mmiliki wa TP Mazembe, Moise Katumbi. Juhudi za kumtafuta zilifanyika kumueleza jambo hilo la kumuachia Mbwana kwa mkopo lakini ikashindikana kabisa.
“Kutokana na hali hiyo, basi ikawa imeshindikana na sasa Mbwana atarejea nyumbani Dar es Salaam na baadaye TP Mazembe,” alisema Kisongo.Samatta alifanya mazoezi na kikosi hicho cha CSKA Moscow na kuonyesha uwezo mzuri lakini hata hivyo hakuendelea na mazoezi baada ya taarifa kueleza kwamba aliumia enka. CREDIT GPL


No comments:
Post a Comment