
Tume ya
Taifa ya Uchaguzi(NEC) ikisisitiza kuwa ratiba ya uboreshaji wa daftari
la kudumu la wapiga kura itaenda kama ilivyopangwa, kamati kuu ya chama
cha Demokrasi na Maendeleo imesema itachukua maamuzi magumu endapo
shughuli za uboreshaji huo zitachelewa na kuharibu mchakato wa kura ya
maoni.
Jana,
Mkurugenzi wa NEC, Julius Malaba alisema uboreshaji utaanza Februari 16
kama ilivyotangazwa awali na utamalizika kwa wakati ili kupisha ratiba
ya kura ya maoni.
“Ratiba
inazingatiwa, vifaa vitafika kwa wakati na kuanza kazi kwa wakati,”
alisema Malaba.Akizungumza wakati wa kikao cha dharura cha Kamati Kuu ya
Chadema, Afisa Habari wa Chadema, Tumaini Makene amesema chama hicho
kimeitisha kikao hicho ili kujadili hatma ya uboreshaji wa daftari hilo
na muda uliobaki kabla ya kupiga kura ya maoni Aprili 30, mwaka huu.
Pia
Chadema walisema kuwa watachukua hatua zaidi iwapo mashine za Biometric
Voters Registration(BVR) zitabainika kuwa na kasoro katika uboreshaji
huo. Zoezi la kuandikisha Watanzania milioni 26 wenye sifa ya kupiga
kura lilitakiwa kuanza mwezi huu lakini Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec)
imesema zoezi hilo litaanza Februari 16, mwaka huu kwa sababu bado
inasubiri mashine 7,750 za (BVR) kwa ajili ya kazi hiyo.
“Kwa
mazingira ya kawaida muda uliobaki kwa ajili ya kazi hiyo kubwa hautoshi
ndiyo maana kuitishwa kwa kikao cha dharura ili kufanya uamuzi,”alisema
Makene.
Chanzo: Mwananchi


No comments:
Post a Comment