| Dk.Hussein
NATIONAL BANK OF COMMERCE
BENKI YA TAIFA YA BIASHARA
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Dk
Hussein ateuliwa kuwa mwenyekiti wa muda wa Bodi ya Wakurugenzi ya NBC
JANUARI 22, 2015
Dar es Salaam: Benki ya Taifa ya Biashara
(NBC) imemteua Dk Kassim Hussein kuwa mwenyekiti wa muda wa bodi ya
wakurugenzi.
Hatua hiyo imetokana na kuteuliwa kwa aliyekuwa
mwenyekiti wa bodi ya benki hiyo, Profesa Mussa Assad, kuwa Mdhibiti na Mkaguzi
Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania .
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari iliyotolewa
jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa Muda wa NBC, Bwana Pius
Tibazarwa alisema Dk Hussein atashika wadhifa wa uenyekiti wa bodi ya benki
hiyo mpaka pale atakapoteuliwa mwenyekiti wa kudumu wa bodi hiyo.
Dk Hussein ni mhadhiri mwandamizi katika masomo ya kibenki
na ya fedha katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha (Institute of Finance Management
– IFM) cha Dar es Salaam. Dk Hussein ni msomi mwenye Digrii ya Uzamivu katika
masomo ya kibenki na Digrii ya Uzamili katika masomo ya fedha. Aliteuliwa kuwa
mjumbe wa bodi ya Wakaurugenzi wa NBC tangu mwaka 2010.
“Kwa mara nyingine tena, tunampongeza Profesa Assad
kwa kuteuliwa kwake na kumtakia kila la kheri katika kazi hiyo. Tunamshukuru
pia kwa utumishi wake uliotukuka katika kipindi chake kama mwenyekiti wa bodi
ya Wakurugenzi ya NBC. NBC itaendelea kushirikiana nae kuimarisha uwazi na
uwajibikaji katika sekta ya fedha hapa nchini. Wakati huo huo, tunamtakia kila
la kheri Dk Hussein katika nafasi yake mpya ya uenyekiti wa bodi ya NBC,”
alisema Tibazarwa.
Profesa
Assad aliteuliwa kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali ya Jamhuri
ya Muungano ya Tanzania mnamo mwezi Novemba 2014 baada ya kuitumikia NBC kama
mwenyekiti wa bodi tangu mwaka 2006.
|
January 23, 2015
DK.HUSSEIN ATEULIWA KUWA MWENYEKITI WA MUDA WA BENKI YA NBC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)


No comments:
Post a Comment