| Msimamizi wa bodi ya michezo
ya kubahatisha,Mrisho Millao(kulia)akiandika namba ya Hynes Petro Kanumba (20) Mkazi wa kijiji cha Inyonga mkoani Rukwa aliyeibuka mshindi
wa Shilingi Milioni 10/- katika droo ya nane kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,wengine katika picha kutoka kushoto
Meneja Uhusiano wa Umma wa kampuni hiyo,Matina Nkurlu na
Meneja uhakiki wa mapato Vodacom Zakaria Kamweru.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda
15544.
MAMA MKULIMA ASHINDA MIL. 10/- ZA PROMOSHENI YA JAYMILLIONS YA VODACOM
Mkazi
wa kijiji cha Inyonga Mkoani Rukwa Hyness Petro Kanumba (20) leo
ameibuka mshindi wa kwanza wa Milioni 10 katika droo ya nane ya
promosheni
ya Jaymilions inayoendeshwa na kampuni ya mawasiliano ya Vodacom
Tanzania.
Hyness
ambaye ni mama mwenye mtoto mmoja pia mkulima amesema kuwa amepokea
taarifa hizo kwa furaha akiwa shambani katika kazi zake za kilimo,
kwa kuwa anaamini Mungu amemuona na kwa ushindi huu utabadilisha maisha
yake kwa kiasi kikubwa.
“Kwa
muda mrefu nimekuwa nikihangaika na kazi za kilimo na kukumbana na
changamoto nyingi kama vile ukosefu wa masoko ya mazao ,pembajeo
za kisasa .Kwa ushindi huu naamini nitaboresha shughuli zangu za kilimo
ikiwemo kuanzisha biashara ndogo na kuboresha makazi yetu,nashukuru
Vodacom kwa kuanzisha promosheni hii”.Alisema Hynes kwa furaha.
Akiongea
muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi,Meneja Uhusiano wa Umma wa
Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu amempongeza mshindi na kuwahimiza
wateja wote wa Vodacom kuchangamkia promosheni hii kwa kuhakikisha
wametuma neno JAY kwenda namba 15544 ili kutopoteza nafasi zao za
kushinda.
Alisema
kuwa tangu promosheni hii ianze mapema mwezi huu tayari wateja watano
wamejishindia shilingi milioni moja kila mmoja na maelfu
wengine tayari wamejishindia muda wa maongezi.
“Promosheni
hii itadumu kwa muda wa siku mia moja hivyo leo ni droo ya nane hivyo
bado kuna mamilioni ya fedha yamewasubiri watanzania,wanachopaswa
kufanya ni kuhakikisha
kila siku wameangalia kama namba zao zimeibuka kwenye droo ya siku kwa
kutuma neno Jay kwenda namba 15544. Promosheni hii inayoendelea ya
Jaymillions inawahusisha wateja wote wa Vodacom,kiasi kikubwa
cha fedha kitaendelea kutolewa kila siku na ni rahisi kabisa kila mtu
kushiriki. Mara tu ujumbe huu unapotumwa, mteja atapokea ujumbe mfupi
utakaomjulisha kama ameshinda na ikiwa hajashinda
siku hiyo atajulishwa hivyo na kuambiwa ajaribu tena siku inayofuata.
Kila SMS itagharimu Sh. 300/- tu”.Alisema.
Vodacom
imepanga kutoa mshindi mmoja wa Sh. 100m/-, washindi kumi wa Sh. 10m/-
na washindi thelathini wa Sh. 1m/- KILA SIKU kwa siku mia moja! Pia
washindi
elfu kumi watapokea muda wa maongezi wa bure wenye thamani ya Sh.
1000/-
|
| Meneja Uhusiano wa Umma wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(katikati)akiongea na mshindi wa shilingi Milioni 10/- Hynes Petro Kanumba (20) Mkazi wa kijiji cha Inyonga mkoani Rukwa,aliyeibuka na ushindi huo katika droo ya nane kupitia promosheni ya JayMillions inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,kushoto ni Msimamizi wa bodi ya michezo ya kubahatisha,Mrisho Millao na Meneja wa huduma za ziada wa kampuni hiyo Mathew Kampambe.Ili mteja kujua kama ameshinda anatakiwa kutuma neno Jay kwenda 15544. |


No comments:
Post a Comment