KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

January 23, 2015

KATIBU MKUU WA CCM NDUGU ABDULRAHMAN KINANA AENDELEA NA ZIARA UNGUJA KASKAZINI

4
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndugu Vuai Ali Vuai naye akishiriki kupanda migomba wakati  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipokitembelea kikundi hicho na kujionea shughuli zao za uzalishaji wa mazao ya kilimo.
1
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Ndugu Vuai Ali Vuai mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Kikobweni jimbo la Chaani mkoa wa Unguja Kaskazini  akiwa katika ziara ya kukagua na kuhimiza utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 inayotekelezwa na serikali ikiwa ni pamoja  kuhimiza uhai wa Chama Cha Mapinduzi mahali ambapo kimelegalega na kuongeza nguvu mahali ambapo kinatekeleza vizuri ilani ya uchaguzi, Katika ziara hiyo Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA FULLSHANGWE-UNGUJA KASKAZINI).
2
Nape Nnauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akielekea kwenye ukubi wa Mkorea mahali ambapo mkutano wa Halmashauri kuu ya Wilaya ya Unguja Kaskazini umefanyika.
3
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki shughuli za kupanda migomba wakati alipokitembelea kikundi cha akina mama cha  Tuko Imara kinachojishughulisha na shughuli za kilimo cha Migomba, Mbogambona na Mananasi katika kijiji cha  Banda Maji.  
 

No comments:

Post a Comment