![]() |
| Kamanda Kidavashari |
MWENYEKITI wa kitongoji cha Songambele katika wilaya ya Mlele mkoani Katavi
kupitia chama cha ACT, Richald Madirisha (31) ameuawa kwa kuchinjwa na
kiwiliwili chake kutenganishwa akituhumiwa kunyang’anya mke wa mtu.
Baada ya mauaji hayo, viungo vyake vya mwili vikiwamo mikono, kichwa, miguu
na sehemu zake za siri vilichemshwa kwenye sufuria mithili ya nyama inavyopikwa
nje ya nyumba yake.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, amethibitisha
kutokea kwa mkasa huo na kuongeza kuwa mauaji hayo yalifanyika juzi saa tano na
nusu usiku nyumbani kwa marehemu katika kitongoji hicho cha Songambele.
Kamanda Kidavashari alisema hayo jana alipozungumza na mwandishi wa
habari hizi kwa simu mjini Mpanda mkoani Katavi. “Uchunguzi wa awali umebaini
kuwa chanzo cha mauaji kimetokana na visa vya marehemu na mtu mmoja, ambaye
walikuwa wakiishi pamoja ambaye alikuwa akimtuhumu marehemu kuwa amemnyang’anya
mwanamke ambaye alikuwa na uhusiano naye kimapenzi.
“Madirisha aliamua kuhama naye kijijini hapo na kuhamia naye kijiji cha
Songambele katika wilaya Mlele,” alisema Kamanda Kidavashari.
Kwa mujibu wa Kamanda Kidavashari, siku ya tukio Madirisha alikuwa
amelala nyumbani kwake akiwa na mkewe aitwaye Mekilina Mussa, lakini ghafla
walitokea watu watano ambao hawafahamiki na kuvunja mlango kisha waliingia
ndani ya nyumba. Inadaiwa kuwa watu hao waliokuwa wameshika mapanga, waliingia
ndani ya nyumba na kuvamia chumba na kumlazimisha mke ajifunike shuka usoni na
alale kitandani.
Baada ya mkewe kujifunika na shuka usoni, inadaiwa watu hao walianza kumchinja
shingo Madirisha kwa kutumia panga huku mkewe akisikia jinsi mumewe alivyokuwa
akilia kwa uchungu.
Kamanda Kidavashari alieleza kuwa baada ya kumchinja shingo, walichukua
kichwa chake na kukiweka kwenye sufuria na kuweka maji ndani ya sufuria na kutoka
nacho nje na kukipika kwenye moto ambao ulikuwa ukiwaka nje ya nyumba ya
Madirisha.
Baada ya hapo, inadaiwa watu hao walirudi ndani ya nyumba na kumnyofoa
sehemu za siri marehemu, mikono yake na nyayo za miguu, kisha waliziweka kwenye
sufuria jingine na kuvipika kwenye moto.
Baada ya unyama huo, kwa mujibu wa madai ya Kamanda Kidavashari, watu
hao waliondoka na kutokomea kusikojulikana huku wakiacha viungo hivyo vya
marehemu vikiendelea kuchemka ndani ya masufuria hayo.
Kidavashari alisema mke wa marehemu baada ya kuona watu hao wametokomea,
alitoka nje na kwenda kutoa taarifa kwa majirani ambao walifika kwenye eneo
hilo na kukuta viungo hivyo vikiendelea kuchemka kwenye masufuria hayo, huku
kiwiliwili chake kikiwa ndani ya chumba chake.
Tayari watu watatu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo, kwa
tuhuma za kuhusika na mauaji hayo ya kikatili



No comments:
Post a Comment