KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

January 25, 2015

MGOMO WA DALADALA UMELETA USUMBUFU MWANZA

MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo
DC Magesa

WAKAZI wa jiji la Mwanza jana wamekumbana na taharuki baada ya barabara ya Nyerere kushindwa kupitika kufuatia madereva wa daladala yanayofanya safari zake kati ya Airport, Bwiru – Igoma/Kishiri kuegesha kwenye barabara hiyo hivyo kusababisha msongamano wa magari.Kuegeshwa kwa daladala hizo kunatokana na kutotakiwa kuegesha katika stendi yao ya awali na badala yake kutakiwa kupitiliza yanapotoka Igoma kwenda Bwiru ama Airport.Wakati daladala hizo zikigoma na kuziba njia katika barabara ya Nyerere, juzi magari ya mizigo yaliziba barabara ya Pamba baada ya kuamuriwa kuondoka katika maegesho yao ya awali ya Tanganyika kupisha wafanyabiashara ndogo maarufu kama machinga.
Hali hiyo imesababisha msongamano wa magari kwenye barabara mbalimbali za jiji hapa wakati madereva wakitafuta njia cha mkato kuepukana na msongamano huo.Mmoja wa waathirika wa msongamano huo Odera Charles aliyekuwa akielekea Nyakato alisema amekuwepo kwenye msongamano huo kwa saa takribani nne baada ya safari yake kuishia barabara ya Nyerere akitokea Nyegezi.
Akizungumza na gazeti hili Mwenyekiti wa Madereva wa daladala, Dede Petro alisema madereva wamefikia uamuzi wa kuegesha magari yao barabarani baada ya stendi yao ya Mwaloni kugawiwa kwa wafanyabiashara ndogo ‘machinga’ na uongozi wa halmashauri ya jiji.Alisema kwa kuwa walionekana hawana thamani mbele ya jamii waliamua kufunga njia hadi muafaka uweze kupatikana baina yao na Halmashauri ya Jiji.Dede alitumia nafasi hiyo kuwaomba radhi wananchi wa jiji la Mwanza walioathirika na uamuzi wao hivyo kukosa huduma kwa zaidi ya saa 6 kwani walilazimika kufanya hivyo ili muafaka uweze kupatikana na huduma ya usafiri iweze kurejea katika hali ya kawaida.

No comments:

Post a Comment