Msaidizi wa nyumbani mwenye umri wa
miaka 18 katika mtaa wa Zimmerman, jijini Nairobi anakabiliwa na
mashtaka baada ya kukiri kumlazimisha mvulana wa miaka mitatu kulamba
sehemu zake nyeti.
Kwa mujibu wa jarida la The Nairobian nchini
Kenya, mamaake mtoto huyo anasema kuwa mwanawe alionekana
kuchanganyikiwa kila mara alipotoka kazini swala lililomlazimu kufanya
uchunguzi.
Alipomuuliza mwanawe,alisema kwamba msaidizi huyo wa nyumbani alikuwa akimnyanyasa kijinsia.
Inadaiwa kuwa msichana huyo alikuwa akimlazimisha mvulana huyo kumramba sehemu zake za siri wakati mama yake anapoondoka.
Mfanyikazi huyo wa miaka 18 alikiri kufanya kitendo hicho kwa kuwa hakupewa mda wa mapumziko lakini akaomba kusamehewa.
Kwa
sasa anakabiliwa na mashtaka ya kunajisi na amewachiliwa kwa dhamana ya
shilingi millioni moja.Kisa hicho kinajiri baada ya kijakazi mwengine
nchini Uganda kufungwa jela baada ya kupatikana katika kanda ya video
akimnyanyasa kwa kumpiga mtoto mdogo. BBC


No comments:
Post a Comment