
Mchezaji Max Gradel wa Ivory Coast
alifunga bao la dakika za mwisho la kipindi cha pili cha mchezo dhidi ya
Mali na hivyobasi kuimarisha matumaini yao ya kufuzu katika robo
fainali ya michuano ya mataifa ya Afrika.
Mali ilikuwa kifua mbele
huku ikiwa na ishara zote za kuibuka mshindi baada ya Bakary Sako
kufunga bao zuri kunako dakika ya saba ya kipindi cha kwanza.
Lakini Gradel alisawazisha katika dakika ya 86 ndani ya eneo la hatari.
Awali
Ivory Coast ilinyimwa penalti ya wazi baada ya Wilfried Bonny kuchezewa
visivyo na Molla Wague huku Kolo Toure pia akikosa bao la wazi.


No comments:
Post a Comment