Nape Nauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akiongozana na Vuai
Ali Vuai Naibu Katibu Mkuu Zanzibar mara baada ya kuwasili ofisi kuu ya
CCM Kiembesamaki mkoa wa Mjini Magharibi.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na
wajumbe mbalimbali na wa wana CCM wakati alipowasili wilaya ya
Kiembesamaki wilaya ya Dimani mkoa wa Mjini Magharibi jana.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Magharibi Yusuf Mohamed Yusuf
akimkaribisha Ndugu Abdulrahman Kinana ili kuongea na wajumbe wa
halmashauri ya wilaya ya Dimani.
 |
| Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana
akiongozana na Makamu wa pili wa Rais Zanzibar Balozi Seif Ali Idd mara
baada ya kupokelewa katika Ofisi kuu ya CCM mkoa wa Mjini Magharibi
wilaya ya Dimani Zanzibar akiwa katika ziara ya kikazi ya siku 15 katika
visiwa vya Unguja na Pemba, Katibu Mkuu Kinana anaongozana na Nape
Nauye Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wakikagua utekelezaji wa Ilani ya
Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 ikiwa ni pamoja na kuhimiza uhai wa chama,
Katika mkutano wa ndani akiongea na wajumbe wa mkutano mkuu wa
Halmashauri ya mkoa wa mjini Magharibi Kinana amesema katika mambo
muhimu ambayo kamati za siasa zinatakiwa kuzingatia wakati wa kuteua
wagombea mbalimbali ni Maadili ya viongozi, Ameongeza kwamba kama kuna
kamati ya siasa itakiuka utaratibu huo na ikaonekana kubeba baadhi ya
wagombea basi Kamati Kuu haitasitakufuata utaratibu wa kikatiba na
kuteua kamati ya siasa nyingine ili kuhakikisha haki inatendeka kwa
wagombea wote walioomba uongozi.(PICHA NA KIKOSIKAZI CHA
FULLSHANGWE-DIMANI-MKOA WA MJINI MAGHARIBI -ZANZIBAR) |
No comments:
Post a Comment