
Timu kutoka kote Afrika zimewasili
nchini Equatorial Guinea wakati ambapo mechi za taifa bingwa barani
zitarajiwa kung'oa nanga hii leo ikiwa ni miezi miwili tangu taifa hilo
la afrika ya kati likubali kuandaa mechi hizo.
Morocco ndiyo
iliokuwa iandae kombe hilo lakini badala yake ikaomba kuahirishwa kwake
kutokana na hofu ya kusambaa kwa ugonjwa wa ebola.
Shirikisho la kandanda barani Afrika CAF hata hivyo lilikataa ombi hilo la Morocco
Mkuu
wa CAF (Hicham El Amrani) anasema kuwa kila tahadhari imechukuliwa
nchini Equatorial Guinea kuwalinda watu kutokana na ugonjwa wa ebola.
Mechi ya kwanza itakuwa kati ya wenyeji Equatorial Guinea na Congo


No comments:
Post a Comment