![]() |
| Kamanda Kashai |
Bomu hilo linadaiwa kuwa ni la kutengenezwa kienyeji, kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Frasser Kashai.
Kamanda wa Polisi Mkoa akizungumzia bomu alisema ni la kurushwa kwa mkono na kwamba lilivurumishwa juzi saa 2 usiku, kwenye kibanda cha kutizamia picha za video kilichoko kijiji cha Amboni na kujeruhi watizamaji watano.
Waliojeruhiwa ni Hassan Abdallah (72), Rashid Ally (45), Mrisho Abdi (29) mtoto Juma Mtoo (15) na Abdul Ismael (19) wote wakazi wa kijiji cha Amboni.
Kashai alisema wamelazwa katika hospitali ya mkoa wa Tanga, Bombo wakiwa na majeraha mbalimbali mwilini na kwamba Ally Rashid (25) mkazi wa kijiji hicho anashikiliwa kwa uchunguzi.
Rashid anahusishwa na bomu hilo linalodaiwa ni la kutengeneza kienyeji kwa mujibu wa Kamanda.
Wakizungumzia tukio la bomu hilo, baadhi ya wananchi waliokuwa eneo la tukio walieleza kuwa waliona kitu chenye mwanga angani kabla ya kutua kwenye banda ambalo walikuwemo watu zaidi ya 30 wakifurahia picha za video.
Jeshi la Polisi limewataka wananchi kutokuwa na hofu ya tukio hilo na kwamba hali ya usalama imedhibitiwa huku uchunguzi wa kina ukiendelea na kuhimiza ushirikiano baina ya wananchi na jeshi hilo kukabiliana na uhalifu.



No comments:
Post a Comment