Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akisalimiana na Josephine Kulea kutoka Taasisi ya Samburu Girls ya
nchini Kenya mara baada ya binti huyo kutoa ushuhuda wake kuhusu namna
alivyoathirika na ndoa za utotoni wakati wa mkutano wa Marais na Wakuu
wa nchi za Umoja wa Afrika kuhusu kampeni ya kutokomeza ndoa za utotoni
uliofanyika huko Addis Ababa nchini Ethiopia hivi karibuni. Binti
huyo alijifungua mtoto wake wa kwanza akiwa na umri wa miaka 17.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akisalimiana na Mke wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Mama Ban Soon
Taek wakati wa mkutano wa Marais na Wakuu wa Nchi za Afrika
uliozungumzia kampeni ya kupiga vita ndoa za utotoni barani Afrika
wakati wa kikao cha 24 cha Umoja huo kilichofanyika Addis Ababa hivi karibuni.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete
akisalimiana na Mke wa Rais wa Chad na Mwenyekiti wa Umoja wa Wake wa
Marais na Wakuu wa Nchi za Afrika (OAFLA) Mama Hinda Deby Itno wakati
wa kikao kilichoandaliwa na Jumuia ya Afrika kuzungumzia kampeni ya
kutokomeza ndoa za utotoni barani humo hivi karibuni.





No comments:
Post a Comment