Na Aziza Masoud, Dar es Salaam
CHAMA cha NCCR-Mageuzi kimeitaka Serikali kuwawajibisha wahusika wakuu walioshiriki katika uchotwaji wa fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow wakiwamo waliotoa rushwa ili kufanikisha mchakato huo.
Akizungumza katika ofisi za chama hicho jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu Mosena Nyambabe, alisema Serikali imepeleka mahakamani maofisa wa ngazi za chini waliohusika katika sakata hilo na kuwaacha watu muhimu waliotoa rushwa.
“Mtuhumiwa namba moja ni mtu aliyetoa rushwa, lakini chakushangaza maofisa wadogo ndio wanaofikishwa mahakamani pekee, Serikali iseme huyu ambaye alihusika kugawa hizo fedha atapelekwa lini mahakamani,”alisema Nyambabe.
Alisema hatua za kisheria pia zinapaswa kuchukuliwa kwa wenyeviti wa kamati za kudumu za Bunge pamoja na waliohusika katika mgawo huo kwakuwa kuwajibika kisiasa kwa kujiuzulu katika nyadhifa zao pekee haitoshi.
“NCCR tunataka kujua kwanini baadhi ya waliopokea rushwa kutoka Akaunti ya Tegeta Escrow kupitia akaunti ya Mkombozi wamefikishwa mahakamani,lakini watu wengine kama Profesa Tibaijuka, Chenge, Ngeleja na wengine hawafikishwi mahakamani,”alisema Nyambabe.MTANZANIA

No comments:
Post a Comment