KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

January 31, 2015

MFUKO WA TAIFA WA BIMA YA AFYA NHIF WA SHIRIKI KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA SHERIA NCHINI

1
Emmanuel Sarakyika wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya akimpima shinikizo la damu mmoja wa watumishi wa Mahakama alipotembelea  kupata huduma hiyo katika banda la NHIF kwenye maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja Dar es salaam ambapo Rais Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika sherehe za kilele cha maadhimisho ya siku ya sheria nchini zitakazo fabika februari 04 2015 katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Saalam.
2
Afisa Masoko na Elimu kwa Umma wa NHIF Bi Hawa Duguza akimpima urefu Bw. Ben Kigongola wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu katika banda la NHIF kwenye maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja Dar es salaam.
3
Afisa Matekelezo wa NHIF, Bi. Shazy Amasha akimsikiliza kwa makini mmoja wa wageni kutoka kundi maalumu aliyetembelea banda la NHIF katika maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja Dar es salaam.
4
Afisa Uanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bi. Tamasha Magongo akitoa maelezo ya jinsi ya kujiunga na Mfuko kwa wageni waliotembelea banda la NHIF katika maadhimisho ya Wiki ya Sheria yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment