MBUNGE wa
Kawe, Halima Mdee (Chadema) ametakiwa kuwasilisha ushahidi kuthibitisha
kauli yake ya kumtuhumu Mbunge Bariadi Magharibi, Andrew Chenge (CCM),
kwa ufisadi.
Chenge
alilazimika kuomba utaratibu wa kiti juzi, baada ya Mbunge huyo wa Kawe
kumtaja mara mbili wakati akichangia mjadala wa taarifa za kudumu za
Bunge zilizowasilishwa juzi.
Mara ya
kwanza, Mdee alimhusisha Chenge na mkataba mbovu wa Kampuni ya Ndege
(ATCL) uliosababisha Serikali kuingia hasara ya zaidi ya Sh bilioni 90.
Licha ya
kumtaja kwenye ufisadi huo ambao kwa mujibu wa Mdee, Chenge ndiye
alikuwa Waziri wa Wizara yenye dhamana na ATCL, pia alimtaja kuhusika
katika kashfa nyinginezo ikiwemo suala la utoaji takribani Sh bilioni
200, katika iliyokuwa Akaunti ya Tegeta Escrow ya Benki Kuu (BoT).(P.T)
"Wabunge
tuanze kuchunguzana humu ndani na kushughulikiana,"alisema Mdee na
kutaja kwamba kwa kuanza, waanze na Chenge pamoja na Dk Shukuru Kawambwa
(Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi), akimhusisha kuwa aliwahi
kushika wizara hiyo yenye dhamana na ATCL.
Kauli
hiyo ilimfanya Chenge kusimama na kusema; "kwa heshima zote nimemvumilia
sana mheshimiwa (Mdee) anayechangia hoja hii. Kama ana ushahidi wa hayo
anayosema, kanuni zetu zinatutaka ayawasilishe mbele yako.
"Mimi
ningelipenda Bunge hili liendelee kuwa na heshima yake. Pili naomba
sana, hayo wanayoyasema wawe na ujasiri wa kwenda kuyasemea nje ya
ukumbi huu wa Bunge, wasijifiche kwenye kinga ya Bunge.
"Nina
mengi ya kusema, lakini kwa sababu nimesimama kwa hoja ya utaratibu,
kunitaja moja kwa moja, naomba aweke hoja mezani,"alisema Chenge.
Mwenyekiti
wa Bunge alikubaliana kwamba Mdee awasilishe ushahidi kwa kiti. Hata
hivyo Mdee alijibu, "Kuna utaratibu wa kikanuni, vielelezo nikitakiwa
kuleta nitaleta.
"Tunazungumza
hapa matumizi mabovu, mikataba mibovu na wizi wa mali ya umma. Mzee
wangu (Chenge) ni rafiki yangu lakini nimeamua nimfungukie kwa sababu
haya ni mambo makubwa." SOURCE MJENGWA BLOG
No comments:
Post a Comment