Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Monduli (katikati) akiuonyesha ujumbe wa NHC eneo lililotengwa
kwa ajili ya kujenga nyumba ambalo alisema lina miundombinu yote muhimu
ikiwemo umeme na maji.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw.
Nehemia Mchechu akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Wilaya ya Monduli na kuhimiza Halmashauri hiyo kukamilisha ulipiaji wa
nyumba hizo ili Shirika liongeze kasi ya kukamilisha mradi huo.
Hii ni sehemu ya nyumba za makazi
zinazojengwa na NHC Wilayani Monduli kama sehemu ya juhudi za Shirika
hilo za kuwezesha wananchi wengi kumiliki nyumba. Nyumba hizi zinajengwa
na NHC katika maeneo mbalimbali nchini.





No comments:
Post a Comment