KWA MAONI AU USHAURI E-mail: inocomm2014@gmail.com, PIGA SIMU: 0714555668

www.utt-pid.org


TEMBELEA: www.utt-pid.org

January 29, 2015

MWAKYEMBE AFUNGUKA

Dk Harisson Mwakyembe

Arusha. Siku mbili baada kukabidhiwa ofisi na aliyekuwa Waziri wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta, waziri ambaye ameteuliwa kushika nafasi hiyo, Dk Harisson Mwakyembe amewataka Watanzania kuondoa hofu ya kuhamishwa kwake kutoka Wizara ya Uchukuzi, huku akisisitiza kuwa hana nia ya kugombea urais.
Dk Mwakyembe aliwataka wananchi kuondoa hofu kwa sababu utendaji aliouonyesha akiwa Wizara ya Uchukuzi, atauhamishia wizara yake mpya.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na gazeti hili muda mfupi baada ya kuapishwa na Spika wa Bunge la Afrika Mashariki (Eala), Daniel Kidega, Mwakyembe alisema utendaji aliouonyesha katika wizara aliyokuwamo awali zamani, ndiyo uliomshawishi Rais Jakaya Kikwete kumhamishia Wizara ya Afrika Mashariki ili kuongeza kasi ya utekelezaji wa masuala ya jumuiya hiyo.
“Watanzania wanapaswa kuondoa kasumba ya kutaka anayefanya vizuri katika nafasi yake kuendelea kubaki hapo hapo. Hapana! Anayefanya vizuri sehemu moja ni vyema akahamishiwa sehemu nyingine ili akafanye vizuri huko pia,” alisema Mwakyembe na kuongeza:

No comments:

Post a Comment