Mwanablogu Raif Badawi ana majeraha ambayo hayawezi kumruhusu kupewa adhabu nyingine
Saudi Arabia imeahirisha adhabu ya kumchapa viboko mwanablogu Raif Badawi kwa sababu ya afya yake.
Mwanablogu
huyo ambaye pia ni mwanaharakati aliyeanzisha mtandao wa 'Forum Liberal
Saudi Network' ambao sasa umefungwa na serikali, alitarajiwa kuchapwa
viboko 50 hadharani baada ya sala ya Ijumaa hii leo.
Mwezi Mei
mwaka jana, alihukumiwa miaka 10 jela na kuandikiwa adhabu ya mijeledi
1,000 kwa kuitusi dini ya kiisilamu pamoja na kutoitii sheria.
Bwana
Badawi alipokea awamu ya kwanza ya viboko Ijumaa iliyopita huku kesi
yake ikisababisha tuhuma kutoka kwa jamii ya kimataifa dhidi ya Serikali
ya Saudia.BBC



No comments:
Post a Comment